IQNA

Wanamaji wa Manowari za Iran katika Sala ya Ijumaa Tanzania +PICHA

16:44 - October 29, 2016
Habari ID: 3470641
IQNA-Maafisa wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameshiriki katika Sala ya Ijumaa katika mji mkubwa wa Tanzania, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, siku ya Ijumaa, Msafara wa 44 wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, unaojumuisha manowari za Alvand na Bushehr, zilitia nanga katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la safari ya kirafiki nchini Tanzania.

Manoari hizo za Iran zilipokelewa na maafisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamuya Iran nchini Tanzania akiwemo Mwambata wa Utamaduni na vile vile Mkuu wa tawi la Tanzania la Chuo Kikuu cha Kimataifa la Al Mustafa SAW.

Katika mahojiano na IQNA, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bw. Ali Baqeri amesema kamanda wa msafara huo wa manoari za Jeshi la Majini la Iran amefanya mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Majini la Tanzania ambapo wamejadili uhusiano na ushirikiano wa kijeshi na kiusalama baina ya nchi mbili.

Aidha amesema maafisa, wafanyakazi na wanachuo walio katika msafara wa manowari hizo jana Ijumaa walijiunga na Waislamu katika Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika Msikiti wa Ithna Ashari mjini Dar es Salaam.

Imamu wa msikiti huo, Hujjatul Islam Ali Dina amewakaribisha wanamaji hao na kusema Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nguvu ya Kiislamu ambayo ni fahari kwa Waislamu na wale wote wanaodhulumiwa duniani. Aidha ameashiria miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei na kusema, Marekani inahadaa inaposema kuwa inapambana na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh kwani ukweli ni kuwa Marekani ndie muungaji mkono mkuu wa ugaidi.

Baada ya Sala ya Ijumaa, wanamaji wa Iran walijiunga na Waislamu wengine hapo katika dhifa ya chakula cha mchana.

Wiki iliyopita, msafara huo wa 44 wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulinusuru meli mbili za kibiashara za Iran ambazo zilishambuliwa mara tatu na maharamia katika Ghuba ya Aden.

Msafara huo wa 44 uliekelea katika maji ya kimataifa Oktoba 5 kulinda njia za baharini zinazotumiwa na meli za kibiashara.

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran Admeli Habibollah Sayyari alisema mwezi Septemba kuwa, Jeshi la Majini la Iran limesindikiza meli za kibiashara na mafuta zaidi ya 3,200 za Iran na zisizo za Iran katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Jeshi la Wanamaji la Iran limefanikiwa kuzuia hujuma nyingi za maharamia dhidi ya meli za Iran na za kigeni katika maji ya kimataifa.

Katika fremu ya juhudi za kimataifa za kupambana na uharamia, manowari za Jeshi la Majini la Iran zimekuwa zikilinda doria katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi tokea Novemba mwaka 2008. Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Majini IMO limepongeza juhudi za Iran za kukabiliana na maharamia.

Wanamaji wa Manowari za Iran katika Sala ya Ijumaa Tanzania +PICHA

Wanamaji wa Manowari za Iran katika Sala ya Ijumaa Tanzania +PICHA

Wanamaji wa Manowari za Iran katika Sala ya Ijumaa Tanzania +PICHA

Wanamaji wa Manowari za Iran katika Sala ya Ijumaa Tanzania +PICHA

Wanamaji wa Manowari za Iran katika Sala ya Ijumaa Tanzania +PICHA


3541497

captcha