IQNA

Bondia Mashuhuri wa Uingereza, Tyson Fury, asilimu

21:21 - November 13, 2016
1
Habari ID: 3470674
IQNA-Bondia mashuhuri wa Uingereza 'Tyson Fury' ametangaza kusilimu kupitia ujumbe wake wa Twitter na kutangaa jina lake kuwa, Riyadh Tyson Mohammad.

Kwa mujibu wa gazeti la Express la nchini Uingereza, Tyson amesambaza picha katika mitandao ya kijamii akiwa amevaa vazi la Kiislamu la kanzu huku akiwa ameinua mikono kusoma duaa.

Katika ujumbe wake chini ya picha hiyo kwenye Twitter, mwanamasumbwi huyo aliyeikumbatia dini tukufu ya Kiislamu maishani ameandika: "Umoja wa dini zote, dunia iliyobarikiwa na Nabii Issa, juhudi za kuishi kwa mujibu wa mafundisho ya Mwenyezi Mungu."

Wafuasi wake wanasema Riyadh Tyson Mohammad anajaribu kufuata nyayo za Mmarekani hayati bingwa wa dunia Muhammad Ali aliyejuliakana kama Cassius Clay kabla ya kusilimuwa mwaka 1964.

Katika kujibu kauli hiyo amesema: "Cassius Clay alibadilika na kuwa Muhammad Ali na baad aya miaka 50 Fury sasa ni Riyadh Muhammad.

3545614

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
eddy
0
0
mungu amrehemu
captcha