John McKissick, Mkuu wa Shirika la
Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kusini mwa Bangladesh
ametangaza kuwa, jeshi la Myanmar na viongozi wa serikali ya nchi hiyo
wamekuwa wakiwalazimisha Waislamu wa jamii ya Rohingya kuyahama makazi
yao na kukimbilia katika nchi jirani. Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa serikali ya Myanmar inatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu.
McKissick amesema Jeshi la Bangladesh limekuwa likuwaua wanaume, likiwachinja watoto pamoja na kuwanajisi wanawake sambamba na kuteketeza na kupora nyumba na kuwalazimisha watu kuvuka mto kuelekea nchi jirani ya Bangladesh.
Wakati huo huo, Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limeituhumu serikali ya Bangladesh kwamba, imekuwa ikiwarejesha Myanmar kwa nguvu Waislamu wa jamii ya Rohingya. Inaelezwa kuwa, kuna Waislamu takribani laki tano wa jamii ya Rohingya wanaoishi nchini Bangladesh kinyume cha sheria.
Siku chache zilizopita mamia ya nyumba za Waislamu wa Myanmar zilichomwa moto magharibi mwa nchi hiyo sambamba na kuendelea ukandamizaji dhidi ya Waislamu hao.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni
jamii ya
wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya
Myanmar
inakataa kuwapa haki za uraia Waislamu ambao idadi yaoni zaidi ya
watu milioni moja na laki tatu. Mabudhha wenye misimamo mikali Myanmar
wanashirikiana na serikali katika kuwakandamiza, kuwatesa na kuwaua
kiholela Waislamu.
Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesia.
3548702