IQNA

Sherehe za Maulidi ya Mtume SAW zaanza nchini Canada

11:23 - December 10, 2016
1
Habari ID: 3470731
IQNA: Waislamu nchini Canada katika eneo la Peel, mkoa wa Ontario wameanza sherehe za Maulidi ya Mtume Muhammad SAW, Mtume wa Rehema kwa walimwengu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Baraza la Ahul Sunna Canada tawi la Peel liliandaa sherehe za Milad-un-Nabii siki za Jumamosi na Jumapili iliyipita.

Aidha sherehe zingine za Maulidi ya Mtume SAW  zinafanyika Jumamosi 10 Disemba katika mji wa  Mississauga chini ya usimamizi wa Jame al Mustafa huku  Jumapili 11 Disemba kukitarajiwa kuwa na sherehe zingine katika Masjidul Aqsa mjini Brampton.

Mnamo tarhe 16 Disemba kituo cha Waislamu wa Pakistan mjini Mississauga vituo vingine vya Kiislamu vimepanga sherehe za Maulidi ya Mtume SAW.  Katika siku ya takayofuata ya Disemba 17 kutakuwa na sherehe kubwa ya Maulidi katika Jamia Riyadhul Jannah na Imdadul Islamic Jamat. 
Januari 7 mwakani Waislamu wa kituo cha Baraza la  Roohani wamepanga sherehe ya Maulid mjini Mississauga.
Aidha katika kipindi cha wikendi kadhaa zijazo kutakuwa na sherehe za Maulidi ya Mtume SAW katika maeneo mbali mbali ya Canada.

Waislamu Canada pia wanajiunga  na wenzao katiak nchi za Ulaya na Marekani katika kampeni maalumu  ya kuwazawadia wananchi maua ya waridi na kadi zenye ujumbe wa amani sambamba na kuwahimiza kuzungumza na Waislamu na kuuliza maswali ili kuondoa dhana potovu zilizopo.

Sherehe za Kimataifa za Mawlid zinafanyika kwa mwaka wa tano mfululizo ambapo Waislamu hubeba maua ya waridi yenye ujumbe wa Mtume Muhammad SAW kuhusu amani, mapenzi na rehema hufikishwa kwa jamii katika miji mikubwa na midogo maeneo mbali mbali duniani.

3552151
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Nurdin salim mwayagah
0
0
ALLAH atuonyeshe haki natuweze kungata in Sha Allah
captcha