IQNA

Rais wa Romania akataa uteuzi wa waziri mkuu Mwislamu

18:48 - December 28, 2016
Habari ID: 3470764
IQNA: Rais wa Romania amepinga uteuzi wa Mwislamu kuwa waziri mkuu katika nchi hiyo ya Ulaya mashariki.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Rais Klaus Iohannsi amesema amechunguza kwa kina kauli zote za kuunga mkono na kuping uteuzi wa Bi.Sevil Shhaideh kama waziri mkuu na kuamua kutokubali uteuzi huo. Imedokezwa kuwa baadhi ya wapinzani wa Shhahide wanasema anamuunga mkono Rais Bashar al Assad wa Syria na Harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Bi. Shhaideh ni kutoka kabila la Tartar ambao ni wachache nchini humo na jina lake lilikuwa limependekezwa na Chama cha Social Democrats, ambacho kilipata ushindi katika uchaguzi wa bunge mapmea mwezi huu kujinyakulia asilimia 45 ya kura.

Alikuwa ameteuliwa na kiongozi wa chama Liviu Dragnea ambaye alipaswa kuchukua wadhifa huo lakini hawezi kufanya hivyo kutokana na kuwa aliwahi kupatikana na kosa la dosari za uchaguzi.

Rais Iohannsi ametaka Chama cha Social Democrats kumteua mgombea mwingine kwa nafasi hiyo paisna kutaja sababu ya kumkataa Bi. Shhaideh. Dragnea amesema atapinga uamuzi wa rais kupinga uteuzi huo na kusema, 'watakutana sehemu nyingine' kutatua mzozo huo. Imedokezwa kuwa Chama cha Social Democrat kitaanzisha mkakati wa kutaka kumuondoa Iohannis katika cheo cha urais.

Bi. Shhaideh, 52, ni mwanachama wa Chama cha Social Democrats lakini hakugombea katika uchaguzi wa Disemba moja. Alikuwa waziri wa ustawi wa kieneo kwa muda wa miezi sita mwaka 2015 na hivi sasa ni afisa wa ngazi za juu katika wizara hiyo.

/3557255

captcha