Ayatullah Hashemi Rafsanjani amepata mshtuko wa moyo leo Jumapili
usiku katika hospitali moja Tehran na madaktari wamejitahidi kumpa matibabu ya
haraka lakini hawakufanikiwa.
Hashemi Rafsanjani, ambaye ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 82,
alijiunga na chuo cha kidini akiwa kijana na kuanza masomo ya kidini hadi
kufikia daraja ya Ijtihad.
Tokea mwaka 1958 alijiunga na mapambano dhidi ya utawala wa
kiimla wa Shah ambapo alifungwa jela mara saba na kuendeleza mapambano
hayo hadi wakati wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979.
Ayatullah Rafsanjani alikuwa mwenye azma imara katika harakati ya
Mapambano ya Kiislamu yaliyoongozwa na Imam Khomeini MA.
Kati ya nyadhifa ambazo Ayatullah Rafsanjani aliwahi kushika baada
ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran, Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi wa Mapinduzi ya
Kiislamu, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, Kaimu Amri
Jeshi Mkuu, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Ulinzi wa Kitaifa na nafasi aliyoishika
hadi kifo chake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa
Kiislamu.
Viongozi mbali mbali wa Iran na wananchi wametuma salamau za rambi
rambi kufuatia kifo cha Ayatullah Rafsanjani. Mazishi ya mwanazuoni huyo wa
Kiislau na mwanampainduzi yamepangwa kufanyika Jumanne mjini Tehran.