IQNA

Utawala wa Aal Khalifa wawanyonga vijana watatu Wabahraini

14:50 - January 15, 2017
Habari ID: 3470796
IQNA-Utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain umewanyonga vijana watatu kwa madai ya kuupinga utawala wa kiimla katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.
Utawala wa Aal Khalifa wawanyonga vijana watatu Wabahraini

Taarifa zinasema hukumu hizo za kifo zimetekelezwa mapema leo asubuhi jambo ambalo limeibua maandamano ya wananchi wenye hasira katika maeneo ya Diraz, Bani Jamra na Sanabis.

Askari wa utawala wa Aal Khalifa walijaribu kuyazima maandamano kwa kutumia risasi za plastiki na gesi ya kutoa machozi.

Wakuu wa Manama pia wamewazuia wananchi kushiriki katika mazishi ya vijana walionyongwa kidhalimu.

Mtandao wa habari wa Lu'lu, umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wananchi wengi wa Bahrain wameandamana mapema leo asubuhi kupinga hukumu hiyo.

Tarehe 9 mwezi huu wa Januari, mahakama ya rufaa ya Bahrain ilipasisha hukumu ya kunyongwa vijana hao watatu kwa madai ya kuhusika na mauaji ya maafisa wa polisi na kutega bomu, licha ya vijana hao kukanusha vikali madai hayo.

Vijana walionyongwa na kufa shahidi ni Sami Mushaima, Abbas Jamil Tahir al-Sami’ and Ali Abdulshahid al-Singace. Mnamo Januari 9 mahakama ya rufaa ya ukoo wa Aal Khalifa ilipinga rufaa ya viajana hao wanaharakati wa demokrasia.

Tokea Februari mwaka 2011, Bahrain imekuwa ikishuhudia mwamko wa Kiislamu ambapo wananchi wanataka kuwa na haki ya kuwachagua viongozi na kuwepo usawa na uadilifu katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi. Utawala Bahrain, ambao ni muitifaki mkubwa wa Marekani na Uingereza, umekuwa ukikandamiza maandamano ya ambani ambapo idadi kubwa ya watu wameuawa, mamia kujeruhiwa na wengine wengi kushikiliwa gerezani.

http://iqna.ir/fa/news/3562825

Kishikizo: iqna aal khalifa bahrain
captcha