IQNA

Rais wa Sudan adai Iran inaeneza Ushia Afrika ili apate msaada wa Saudia

16:24 - January 27, 2017
Habari ID: 3470816
IQNA-Rais Omar al Bashir w Sudan ametoa madai yasiyo na msingi wowote kuwa eti Iran inaeneza madhehebu ya Shia barani Afrika.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Rais al Bashir, ambaye siku chache zilizopita alitembelea Saudi Arabia na kukutana na mfalme wa nchi hiyo, amefanya mahojiano na gazeti la Kisaudi la Sharq al Awsat na kudai kuwa eti Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalenga kueneza satwa na ushawishi wake katika nchi zote za Kiarabu.

Katika madai ambaye yanaonekana kutolewa kwa ili kupata misaada zaidi kutoka utawala wa kiimla wa Saudi Arabia, al Bashir ameithuhumu Iran kuwa inalenga kueneza madhehebu ya Shia barani Afrika. Aidha ameendelea kudai kuwa eti Iran ilikuwa inataka kueneza Ushia nchini Sudan.

Omar al Bashir ametoa madai hayo yasiyo na msingi katika hali ambayo Iran iko mstari wa mbele katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikiendeleza jitihada zisizo na kikomo katika uga wa kukabiliana na ugaidi na makundi ya wakufurishaji wenye misimamo mikali na hivyo kufanikiwa kudhoofisha makundi hayo na kuyazuia kuenea kaskazini mwa Afrika.

Tarehe 23 Januari al Bashir alitembelea Saudia kwa safari rasmi na kukutana na mtawala wa nchi hiyo, Salman bin Abdulaziz. Ikumbukwe Januari mwaka 2016, Sudan ilichukua hatua ya upande moja na kukata uhusiano wake na Iran baada ya kuhongwa na Saudia kufanya hivyo.

Hivi karibuni, Marekani iliiondolea Sudan vikwazo kufuatia ombi la Saudia kama njia ya kumshukuru Omar al Bashir kwa kuvunja uhusiano na Iran.

Hivi sasa ili kujipendekeza zaidi kwa mabwana zake katika kasri za ukoo wa Aal Saudi, dikteta Omar al Bashir anatumia kila fursa kuituhumu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

3567246

captcha