IQNA

Wanawake Waislamu Austria marufuku kuvaa niqabu

18:57 - January 31, 2017
Habari ID: 3470825
IQNA-Serikali ya Austria imechukua hatua ya kuwapiga marufuku wanawake Waislamu kuvaa aina ya hijabu inayofunIka uso wote, maarufu kama niqabu, katika maeneo yote ya umma nchini humo.

Chama tawala cha Austria kimedai kimechukua hatua hiyo kwa kuhofia kuwa chama henye misimamo mikali ya mrengo wa kulia cha Freedom Party kitatumia suala la uvaaji niqabu kuibua hisia dhidi ya wageni na kuingia madarakni kwa wimbi hilo.

Kansela Christian Kerr wa Austria, ambaye anaongoza muungano tawala wa vyama vya Social Democrats (SPOe) na People's Party (OeVP).

Amesema marufuku ya vazi linalofunika uso kikamilifu katika sehemu za umma itatekelezwa hatua kwa hatua katika kipindi cha miezi 18 ijayo.

Idadi ya Waislamu Austria inakadiriwa kuwa laki sita  na Kansela wa nchi hiyo amesema wale ambao hawaridhiki na sheria hiyo  wako huru kuondoka.

Katika miezi ya hivi karibuni, chama hicho cha Freedom Party kinaonekana kuongoza katika uchunguzi wa maoni ikiwa ni muendelezo wa vyama vya kibaguzi kupata umashuhuri Ulaya hasa baada ya ushindi wa Donald Trump kama rais wa Marekani.

Bunge la Ufaransa pia nalo miezi sita iliyopita lilipitisha sheria sawa na hiyo ya Austria ya kupiga marufuku nikabu katika maeneo ya umma. Ubelgiji, na baadhi ya maeneo ya Uholanzi nayo pia yamepiga marufuki vazi hilo.

Naye Kansela Angela Merkel wa Ujerumani pia mwezi uliopita katika kikao cha chama chake cha Wademokrat Wakristo alisema niqabu inayovaliwa na wanawake Waislamu inapaswa kupigwa marufuku katika maeneo ya umma.

Vazi la niqabu ni aina ya Hijabu ambayo huvaliwa na baadhi ya wanawake Waislamu huku wengi wakifadhilisha kuvaa Hijabu ambayo haifuniki uso kikamilifu.

Pamoja na kuwepo chuki hizo dhidi ya Uislamu na Waislamu, ripoti za hivi karibuni za uchunguzi wa maoni katika vyombo vya habari vya Kimagharibi vimesema kwamba vizingiti vinavyowekwa na nchi za Ulaya si tu kuwa havijaudhoofisha Uislamu bali jambo hilo limepelekea kushuhudiwa ongezeko la wanaovutiwa na Uislamu na vazi la Hijab.

3462094
captcha