IQNA

Mwanamke Mwislamu mkaazi wa Uhispania

Nimenyimwa nyumba ya kukodi kwa ajili tu mimi ni Mwislamu

0:03 - February 06, 2017
Habari ID: 3470836
IQNA: Bi. Bushra Ibrahimi ni Mwislamu mkaazi wa Uhispania ambaye anasema Waislamu katika nchi hiyo ya Ulaya wanakumbwa na masaibu mengi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Bi. Bushra anaishi katika Jimbo la Catalonia nchini Uhispania na anasema kuwa kutokana na kuwa yeye ni Mwislamu imekuwa taabu kupata nyumba ya kukodi.

Anasema katika jimbo hilo la kaskazini mashariki mwa Uhispania, kuna ubaguzi wa wazi wazi dhidi ya raia wa kigeni hasa Waislamu na kwamba mwaka polisi ya Catalonia imepokea ripoti nyingi za ubaguzi ambapo aghalabu zimetajwa kuwa ni jinai zilizojiri Barcelona, mji mkuu wa Catalonia.

Bi. Bushra Ibrahimi, mwanamke Mwislamu mwenye kuvaa vazi la staha la Hijabu anaishi Catalonia ambapo anabaguliwa sana kwa ajili ya dini yake. Anafafanua zaidi kuhusu masaibu anayoyapata kwa kusema: "Siwezi kupata nyumba ya kukodi kwa urahisi kote Catalonia. Hii inatokana na kuwa mimi ni Mwislamu na zaidi ya hilo navaa vazi la Hijabu.” Anaongeza kuwa, kila wakati anapopanga miadi ya kuenda kutizama nyumba aitakayo, wahusika wanapofahamu kuwa yeye ni Mwislamu, basi papo hapo wao hubatilisha mkutano huo. Anasema hilo si lolote kwake kwani anapata masaibu mengi zaidi katika eneo lake la kazi kutokana na vazi alivaalo kila siku la Hijabu.

Bushra mwenye umri wa miaka 31 ana asili ya Morocco na kwa muda wa miaka mitatu sasa anaishi Catalonia na ana watoto wane. Anasema: "Awali hali ilikuwa nzuri na wala sikuwa na matatizo ya kukodisha nyumba; lakini Januari mwaka jana matatizo yalianza na ikawa vigumu sana kupata nyumba.”

Mwanamke huyo Mwislamu mwenye kuzingatia mafundisho ya Kiislamu maishani anasema kuwa: "Baadhi ya wenye nyumba wanatangaza wazi wazi kuwa hawataki kuona wahajiri hasa Waislamu wakikodi nyumba zao huku baadhi wakijizuia kutaja sababu za kukataa kuniruhusu nikodi nyumba zao.”

Pamoja na kuwa kuna wakaazi karibu laki tatu Waislamu wahajiri eneo la Catalonia huku kukiwa na Wahispania asili 3000 ambao ni Waislamu, lakini kunashuhudiwa vitendo vingi vya chuki dhidi ya Waislamu.

Haya yanajiri katika hali ambayo Uislamu una historia ndefu nchini Uhispania ambapo nchi hiyo iliwahi kutawaliwa kwa karne kadhaa na Waislamu.Nimenyimwa nyumba ya kukodi kwa ajili tu mimi ni Mwislamu

Msikiti wa kale wa Arcade huko Cordoba, Andalusia, Uhispania

Al-Andalus ilikuwa jina la Kiarabu la sehemu za Rasi ya Iberia (Uhispania na Ureno za leo) zilizotawaliwa kwa karne kadhaa na Waislamu kati ya miaka 711 and 1492 Miladia.

Eneo hilo ilikuwa chini ya falme na watawala mbalimbali kwanza chini ya Banu Umayya, halafu Ukhalifa wa Cordoba (929-1031) na baadaye chini ya milki mbalimbali hasa Wamurabitun (Almoravi) (1073-1147) na Wamuwahidun (Almohad) (1125-1269) kutoka Morocco.

3570744/

captcha