IQNA

Kansela wa Ujerumani ataka Waislamu washirikishwe katika vita dhidi ya ugaidi

15:12 - February 20, 2017
Habari ID: 3470860
IQNA-Kansela wa Ujerumani ametoa mwito wa kushirikishwa Russia na Waislamu katika kukabiliana na jinamizi la ugaidi.

Kadhalika Kansela wa Ujerumani amesisitizia umuhimu wa kujumuishwa jamii ya Waislamu katika vita hivyo, na kubainisha kuwa nchi za Kiislamu zimekuwa zikitengwa katika juhudi hizo licha ya kuwa ndizo wahanga wakuu wa harakati za kigaidi duniani.

Kwengineko katika hotuba yake na kwa njia isiyo ya moja kwa moja, Merkel ameikosoa Marekani kwa kukataa kuzishirikisha nchi zingine katika jitihada za kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinaoikabili dunia, akisisitiza kuwa, matatizo yaliyopo duniani kwa sasa hayawezi kutatuliwa na serikali au nchi moja bila kushirikiana na nchi nyingine.  

Akihutubu katika Mkutano wa 53 wa Usalama wa Munich nchini Ujerumani hapo jana, Merkel alisema ingawaje Ujerumani sawa na nchi nyingine za Magharibi zimekuwa zikitofautiana na misimamo kadha wa kadha ya Russia, lakini ikija katika suala la ugaidi, hakuna budi kuishirikisha Moscow.

Amesema lengo la Russia kama vile nchi zote duniani ni kulitokomeza kikamilifu janga la ugaidi, ambalo limesababisha maafa makubwa katika dunia ya leo.

3462243

captcha