Katika mahojiano maalumu na Kanali ya Kwanza ya Shirika la Utangazaji la Iran IRIB yaliyorushwa hewani Jumatatu usiku, Nasrallah amesisitiza kuwa, Iran inatuma ujumbe mzito wa mshikamano na Palestina kwa kuandaa Kongamano la Kimataifa la Kuunga Mkono Intifada (mwamko) ya Palestina.
Mkutano wa kimataifa wa siku mbili kuhusu kuunga mkono mwamko wa Palestina unaanza leo hapa mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi 80. Sayyed Nasrallah amesema mkutano huo unafanyika katika wakati muhimu wa mabadiliko ya sera za Marekani kuhusu kile kinachotajwa kuwa suluhisho la nchi mbili baina ya Palestina na Israel.