IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Dhulma wanayotendewa Wapalestina inamgusa kila mpigania uhuru, haki na uadilifu

22:36 - February 21, 2017
Habari ID: 3470862
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kisa kilichojaa machungu na kuzijeruhi nyoyo za watu kutokana na dhulma wanayofanyiwa raia wa Palestina wenye uvumilivu, subira na mapambano, kinamgusa kila mwanadamu mpigania uhuru, haki na uadilifu kote duniani.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo mjini Tehran katika ufunguzi wa mkutano wa sita wa kimataifa wa kuunga mkono Intifadha ya Palestina unaofanyika hapa mjini Tehran ambapo sanjari na kusisitizia kuwa, ukandamizaji wa kutisha dhidi ya taifa la Palestina, kamatakamata ya kila mara, mauaji na uporaji, kughusubu ardhi za taifa hilo,  ujenzi wa vitongoji vya walowezi na njama kwa ajili ya kubadilisha muundo na utambulisho wa mji mtukufu wa Quds na Masjidul-Aqsa na maeneo mengine matukufu ya Kiislamu na Kikristo, kunakofanywa na utawala haramu wa Israel kupitia uungaji mkono wa kila upande wa Marekani na baadhi ya madola ya Magharibi, ni mambo ambayo kwa bahati mbaya hayakabiliwi na radiamali yoyote ya walimwengu.

Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa, raia wa Palestina wanajifakharisha kwa kuona kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu yuko pamoja nao na kwamba wamekabidhiwa ujumbe mtukufu wa kutetea ardhi hizo tukufu na Masjidul-Aqsa. Kiongozi Muadhamu amefafanua kuwa, uchunguzi uliofanywa unaonyesha kwamba, katika historia hakuna taifa lolote duniani ambalo limewahi kukumbwa na machungu, mateso na hatua za kidhalimu kutoka ndani na nje ya eneo na kukaliwa kikamilifu kwa mabavu huku raia wake wakitimuliwa majumbani mwao na kisha kuja kundi jingine kukalia maeneo yale kama taifa la Palestina na kwamba, suala hilo ni moja ya mambo ambayo yamechafua na yanaendelea kuchafua kurasa za historia.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu faili hilo la mateso litafungwa. Amesisitiza kuwa kongamano la sita la kimataifa kwa ajili ya kuunga mkono Intifadha ya Palestina linafanyika katika hali ambayo dunia na eneo la Mashariki ya Kati linakabiliwa na hali mbaya. Amebainisha kwamba katika eneo, kwa muda wote Iran imekuwa ikifanya juhudi za kuunga mkono taifa la Palestina katika kupambana na njama za dunia na kutokana na hilo siku hizi eneo hili limekumbwa na machafuko na migogoro mingi. Amesema, migogoro iliyopo sasa katika nchi kadhaa za Kiislamu imepelekea kupungua uungaji mkono kwa suala la Palestina na matukufu ya kuikomboa Quds. Kiongozi Muadhamu amebainisha kwamba uzingatiaji wa migogoro hiyo unaonyesha kwamba madola yenye kupenda makubwa, yameanzisha utawala wa Kizayuni katika eneo hili ili kupitia machafuko makubwa na ya muda mrefu, ziweze kuzuia uthabiti, usalama na maendeleo ya eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa ajili hiyo amesema kuwa licha ya kuwepo tofauti nyingi baina ya nchi za Kiislamu, tofauti ambazo baadhi ni za kawaida na zingine zinazotokana na njama za maadui huku zingine zikiwa zinatokana ma mughafala, lakini kadhia ya Palestina inatakiwa iwe muhimili wa umoja baina yao.

3576729
captcha