IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya vijana yanafanyika Oman

18:36 - February 27, 2017
Habari ID: 3470869
IQNA: Mashindano ya 28 ya Qur'ani na Hadithi kwa ajili ya vijana wa nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi yameanza Februari 26 mjini Muscat, Oman.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yanafanyika katika Msikiti wa Jamia wa Sultan Qaboos na yamewaleta pamoja washiriki 40 kutoka nchi zote sita za baraza hilo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Sheikh Kahlan bin Nabhan Al Kharusi, Naibu Mufti Mkuu wa Oman amesema mashindano kama hayo ya Qur'ani yanalenga kuwahimiza vijana kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu.

Amesema vijana wakilelewa ipasvyo, watakuwa na wana uwezo wa kueneza ujumbe wa Qur'ani na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW.

Muhammad bin Said Almunawari, mkuu wa kamati andalizi ya mashindano hayo amesema kuna makundi ya marika matatu katika mashindano hayo ya Qur'ani yaani miaka 11-16, 16-120 na 21-25.

Amesema mashindano hayo ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani pamoja na kuhifadhi Hadithi yataendelea hadi Machi 3 na ni katika harakati za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.

captcha