1. Msikiti wa Nurda Kamal uko Norilsk kaskazini
mwa Siberia na ulifunguliwa mwaka 1998. Msikiti huo uko katika Kitabu cha Guinness
cha Rekodi za Dunia kwa kuwa msikiti ulio eneo la kaskazini zaidi duniani. 2. Msikiti wa Jamia wa Moscow ni msikiti mkubwa
zaidi barani Ulaya ambao una ghorofa sita na minara yenye urefu wa mita 79 ambayo
ni mirefu zaidi Ulaya. 3. Msikiti wa Samawati ambao uliasisiwa mwaka
1910 katika kisiwa cha Petrogradsky. Huu ni msikiti pekee Ulaya uliojengwa katika
kisiwa kilicho katika mto. 4. Msikiti wa Sultan Delimakhanov ni msikiti
mkubwa zaidi ulio kijijini barani Ulaya na uko katika kijiji cha Dzhalka katika
jimbo la Chehenia. Huu ni msikiti uliojengwa kumuenzi Sultan
Delimkhanov afisa wa kijiji aliyeuawa muongo wa 1990 na unaweza kutumiwa
wakati moja na waumini 5,000
5.
Msikiti wa Jamia wa Derbent, jimbo la Daghestan ulijengwa kati ya mwaka 733 na
734 Miladia na umetajwa kuwa msikiti mkongwe Zaidi Raussia. Msikiti huu uko
katika orodha ya UNESCO ya turathi za dunia.
6.
Msikiti wa Jamia wa Makhachkala katika jimbo la Daghestan ulijengwa mwaka 1997
kupitia ufadhili wa moja ya familia tajiri zaidi
7.
Msikiti wa Kul Sharif wa Kazan ulijengwa sehemu ilimokuwa hekalu adhimu ya Ivan
Groznya iliyoharibiwa katika kampeni zake za kivita mwaka 1547-52. Msikiti huo
una minara sita yenye urefu wa mita 55 na uko katika orodha ya UNESCO ya
turathi za dunia. 8.
Msikiti wa Jamia wa Madrasa Lala-Tulip ulijengwa mwaka 1990-98 kwa usanifu
majengo wa kisasa na una minara pacha yenye urefu wa mita 53.
9.
Msikiti wa Bulgar huko mjini Kazan katika jimbo la Tatarstan na ni msikiti
pekee Russia ambao kuta zake zote zina rangi nyeupe. Msikiti huu pia una nakala
kubwa zaidi ya Qur'ani duniani. 10. Msikiti
wa Ahmad Kadyrov katika
jimbo la Chehnia umetajwa kuwa Moyo wa Chechenia na unashabihiana sana na ule
Msikiti wa Samawati wa Istanbul. Msikiti huo ndio msikiti pekee Russia ambao
taswira zake za video zinarushwa hewani masaa 24 kwa siku