IQNA

Waislamu Amerika Kaskazini wajadili changamoto za Trump

19:51 - April 17, 2017
Habari ID: 3470938
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wa eneo la Amerika Kaskazni wamekutana katika la 42 la kila mwaka ambapo wamejadili changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo katika nchi za Canada na Marekani hasa katika utawala wa Donald Trump.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, taarifa iliyotolewa na ofisi ya Muungano wa Kiislamu ya Amerika Kaskazini (ICNA) , kongamano hilo la siku tatu limejadili kadhia ya 'Juhudi kwa ajili ya Mafanikio ya kweli naUjumbe wa Mungu wa Musa AS, Issa AS na Mtume Muhammad SAW mjiniBaltimore katika jimbo laMaryland, mashariki mwa Marekani.

Aidha ICNA imesisitiza kuwa, katika kongamano hilo kumefanyika pia vikao mbalimbali na kujadili masuala kama vile, kukabiliana na chuki dhidi ya dini ya Kiislamu, kutetea haki za Waislamu katika kipindi cha utawala wa Rais Donald Trump, wa Marekani, ongezeko la jinai dhidi ya Waislamu na hatuahasi ya serikali ya rais huyo ya kuwazuia Waislamu kuingia nchini humo.

Katika kongamano hilo lililanza Ijumaa na kumalizika Jumapili, Waislamu wamepata fursa ya kutoa malalamiko yao kuhusiana na matatizo mbalimbali yanayowakabili ndani ya taifa hilo hususan baada ya kuingia madarakani Rais Trump mwenye misimamo ya kibaguzi na chuki.

Pembizoni mwa kikao hicho, zaidi ya watu 1,000 wasio na makazi walipatiwa misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula, ambayo ilitolewa na kundi la wafuasi wa dini tatu za Uyahudi, Ukristo kwa kushirikiana na Waislamu waBaltimore. ICNA ilianzishwa mwaka 1971 kama jumuiya yenye kuzileta pamoja jumuiya zote za Kiislamu katika eneo la Amerika Kaskazini. ICNA inatafautiana na Jumuiya ya Kiislamu ya Amerika Kaskazni ISNA ambayo nayo pia inazileta pamoja jumuia mbali mbali za Waislamu Amerika Kaskazini.

Takwimu zinaonesha kuwa uhalifu unaosababishwa na chuki hususan dhidi ya Waislamu umeongezeka nchini Marekani tangu Trump achaguliwe kuongoza nchi hiyo.

Wataalamu wanasisitiza kuwa, matamshi ya kibaguziya Trump pamoja na sera zake ni chanzo cha chuki, mashambulizi na hujuma zinazofanywa na makundi ya kibaguzi dhidi ya Waislamu katika miji mbalimbali ya Marekani.

3590000
captcha