IQNA

Tizama Mashindano ya Qur'ani Iran 'Live' katika intaneti

9:20 - April 23, 2017
Habari ID: 3470947
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Iran yanapatikana moja kwa moja au live kwa njia ya mtandao wa kijamii wa Instagram na kupitia televisheni ya qurantv.ir/live.
Tizama Mashindano ya Qur'ani Iran 'Live' katika Instagram kupitia @iqnanews

Mashindano hayo amabyo yalifunguliwa rasmi Jumatano yanawashiriki 270 wakiwemo wasomaji na waliohifadhi Qur'ani tukufu kutoka nchi 83 duniani.

Mashindano yataendelea kwa muda wa siku sita hapa Tehran, hadi Jumanne 26 Aprili inayosadifiana na tarehe 27 Rajab, katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA.

Kwa wale wenye uwezo wa kufuatilia mashindano hayo kupitia intaneti wanaweza kutemebelea ukurasa wa IQNA katika akaunti ya Instagram ya @iqnanews

Aidha unaweza kufuatilia mashindano hayo moja kwa moja kupitia Televisheni ya Qur'ani ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika toovuti ifuatayao

http://qurantv.ir/live

359123

captcha