IQNA

Ustadh Sagar wa Kenya ashika nafasi ya nne mashindano ya Qur'ani Iran

19:53 - April 26, 2017
Habari ID: 3470952
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 34 Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yamemalizika huku Ustadh Haitham Sagar Ahmad wa Kenya akishika nafasi ya nne katika kuhifadhi Qur'ani kikamilfu.

Ustadh Sagar wa Kenya ashika nafasi ya nne mashindano ya Qur'ani IranKaika hafla ambayo imefanyika alasiri hii katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran, Ustadh Sagar ametangazwa wa nne huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Ustadh Musa Muutamidi kutoka Iran, nafasi ya pili Yassir Ahmad wa Syria na nafasi ya tatu Abdullah Muhammad Adam wa Sudan. Nafasi ya tano katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qu'rani imechukuliwa na mwakilishi wa Niger Mohammad Hassan Haroun.

Halikadhalika katika kitengo cha qiraa, mshindi alikuwa ni Ustadh Said Parvizi kutoka Iran, nafasi ya pili Fallah Zalif wa Iraq na nafasi ya tatu Rahmatullah Bayat wa Sweden.

Mbali na mashindano hayo ya kawaida ya wanamume, mwaka huu mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran yalikuwa ya kwanza ya aina yake duniani kwani kwa kipindi cha wiki moja iliyopita pia kumefanyika mashindano maalumu ya Qur'ani ya wanawake na pia ya watu wenye ulemavu wa macho, ya wanachuo wa vyuo vya dini na pia mashindano ya wanafunzi wa shule. Walioshika nafasi ya kwanza hadi ya tano katika mashindano hayo yote wammetunukiwa zawadi za fedha taslimu na zawadi nyinginezo.

Kauli mbiu ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Iran mwaka huu imekuwa ni "Kitabu Kimoja Umma Moja" kwa kuzingatia mafundisho ya Qur'ani Tukufu ya umoja baina ya Waislamu.Ustadh Sagar wa Kenya ashika nafasi ya nne mashindano ya Qur'ani Iran

Mashindano ya kimatiafa ya Qur'ani ya Iran yalianza Alhamisi iliyopita na kumalizika jana Jummane kwa munasaba wa tarehe 27 Rajab ambayo huadhimishwa na Waislamu duniani kama siku ya Israa na Miraj pamoja na kubaathiwa Mtume Muhammad SAW.

Mashindano hayo ya Qur'ani yalikuwa na washiriki 276 kutoka nchi 83 na yamekuwa yakifanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA.

3593638
captcha