IQNA

Qarii wa Qur'ani Indonesia afariki alipokuwa akisoma Surah Al-Mulk+VIDEO

18:04 - April 27, 2017
Habari ID: 3470953
TEHRAN (IQNA)-Kwa hakika hatujui ni wapi na ni lini mauti yatatufikia, hiyo ni siri ya Mola Muumba, Allah SWT.

Qarii wa Qur'ani Tukufu kutoka Indonesia ameaga dunia wakati alipokuwa akisoma Qur'ani Tukufu na hivyo kupata mwisho mwema maishani (husnul khatimah).

Katika video iliyosambaa katika mitandao ya intaneti, Ustadh Ja'afar Abdul Rahman alikuwa anasoma sentensi ya pili ya Surah Al Mulk katika mji wa Surabaya Indonesia siku ya Jumatatu wakati sauti yake ilipoanza kufifia kabla ya kuzimia. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Indonesia, Ustadh Ja'afar aliaga dunia dakika chache baada ya kuzimia.

Qarii huyo alikuwa akisoma Qur'ani katika kikao kilichokuwa kimehudhuriwa pia na Waziri wa Masuala ya Kijamii Indonesia Khofifah Indar Parawansa. Madaktari wanasema alipata mshtuko wa moyo na hivyo kushindwa kumaliza qiraa hiyo.

Ustadh Ja'afar alikuwa msomi mashuhuri wa kidini Indonesia na alikuwa anawavutia wengi kwa qiraa yake nzuri na maridadi ya Qur'ani Tukufu.

Alifariki alipokuwa akisoma Aya ya Pili ya Sura Al Mulk ya Qur'ani Tukufu isemayo: "Ambaye ameumba mauti na uhai kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha."

Tizama clip ya video ya tukio hilo hapa chini.

3462684

captcha