IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kutekeleza mafundisho ya Qur'ani kutaupa heshima umma wa Kiislamu

23:42 - April 27, 2017
Habari ID: 3470954
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesema kuwa kuufahamu na kuufanyia kazi usuli wa Qur'ani wa "Kumwamini Mwenyezi Mungu na kumpinga Shetani" kutaupa izza na heshima umma wa Kiislamu na akaongezea kwa kusema hii leo ulimwengu wa ukafiri umekusudia kufuta utambulisho wa Kiislamu katika kila pembe ya dunia.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ameyasema hayo asubuhi ya leo mjini Tehran alipokutana na walimu, maqarii na mahufadhi wa Qur'ani Tukufu walioshiriki katika Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Qur'ani nchini hapa kutoka nchi 83 za dunia. Amesema kuwa utambulisho wa Kiislamu unazuia uingiliaji na ubeberu wa maadui na kuongeza kuwa, mafundisho ya Qur'ani, ni muokozi na mjengaji wa maisha ya uwezo imara na ya izza kwa umma wa Kiislamu na ni lazima mafundisho hayo yawekwe wazi na kuenezwa katika jamii ya Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesema kuwa, kinachoutanza hii leo umma wa Kiislamu ni "ubeberu wa kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa wa Magharibi" na akafafanua kwamba, leo hii nchi nyingi za Kiislamu hazina "Utambulisho wa Kiislamu", na maadui wanaweza kuingilia utamaduni, imani, uchumi, siasa na mahusiano yao ya kijamii na kuchochea vita na chuki baina ya Waislamu. 

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, kujiweka mbali na Qur'ani kunatoa mwanya kwa maadui wa kupandikiza mbegu za utovu wa imani na utegemezi; na akabainisha kwamba hali ziliyonayo leo serikali za nchi za Kiislamu mkabala na Marekani, Uzayuni na waporaji, inatokana na serikali hizo kujiweka mbali na Qur'an kwani ikiwa tutajikurubisha na kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na utambulisho wa Kiislamu, matatizo yote haya yataondoka.

Kadhalika Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, juhudi za kuieneza na kuifahamu Qur'an, ni moja ya mema makubwa kabisa ambapo sambamba na kusisitiza juu ya udharura wa kuendelezwa harakati za masuala ya Qura'ni nchini Iran amesema kuwa, ni jambo la kusikitisha kuwa mataifa ya Waislamu na nchi za Kiislamu zimejiweka mbali na kitabu hicho cha mbinguni na hazina uelewa wa mafundisho yake halisi. Amesema kuwa, "Kumpinga Taghuti na Kumwamini Mwenyezi Mungu" ni moja ya maana muhimu na yenye kujenga utambulisho ya Qur'an na kwamba, kutiliwa mkazo "Utambulisho wa Kiimani" kuna maana ya kuwekwa mpaka na kujitegemea ili utambulisho huo uweze kujilinda katika kukabiliana na "Utambulisho wa Taghuti na Ukafiri" na kuendelea kupiga hatua zake za maendeleo.

Albamu ya picha za mkutano wa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na walimu, maqarii na mahufadhi wa Qur'ani Tukufu walioshiriki katika Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Qur'ani

Kutekeleza mafundisho ya Qur'ani kutaupa  heshima umma wa Kiislamu


Kutekeleza mafundisho ya Qur'ani kutaupa  heshima umma wa Kiislamu

Kutekeleza mafundisho ya Qur'ani kutaupa  heshima umma wa Kiislamu


Kutekeleza mafundisho ya Qur'ani kutaupa  heshima umma wa Kiislamu

3593700
captcha