IQNA

Mabinti Waislamu wachezaji basketiboli ruhusa kuvaa Hijabu kimataifa

14:55 - May 06, 2017
Habari ID: 3470970
TEHRAN (IQNA)- Shirikisho la Mpira wa Kikapu (basketiboli) Duniani (FIBA) limetangaza kuafiki pendekezo la Iran la kutaka wanawake Waislamu wenye Hijabu kushiriki katika michezo ya kimataifa ya basketiboli).

Mahmoud Mashhoon Mkuu waShirikisho la Mpira wa Kikapu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa, hatimaye Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) limekubaliana na matakwa ya Iran ya wachezaji wake wa kike kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya mpira wa kikapu wakiwa wamejistiri kwa vazi tukufu la Hijabu.

Ameongeza kuwa, uamuzi huo wa FIBA umetangazwa katika kikao cha shirikisho hilo kilichofanyika huko Hong Kong.Mkuu waShirikisho la Mpira wa Kikapu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iranamesema kuwa, kufuatia uamuzi huo, kuanzia Oktoba mwaka huu mabinti wa Kiirani na mabinti Waislamu maeneo mengine duniani sasa wataweza kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya mchezo huo wakiwa wamejistiri kwa vazi la Hijabu.

Ikumbukwe kuwa, Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Kikapu ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa muda sasa haikuwa ikishiriiki katika mashindano ya kimataifa ya mpira wa kikapu kutokana na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) kupiga marufuku wanawake wanaovaa Hijabu kushiriki katika mashindano yanayoandaliwa na shirikisho hilo.

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) lililazimika kuanzisha mchakato wa kuangalia uwezekano wa kuruhusiwa vazi la Hijabu baada ya shirikisho hilo kupokea malalamiko kutoka nchi kadhaa kufuatia marufuku yake ya Hijabu katika mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na shirikisho hilo.

3462755

captcha