IQNA

Waislamu Iceland wanafunga masaa 22 kwa siku katika Mwezi wa Ramadhani

11:17 - June 12, 2017
Habari ID: 3471017
TEHRAN (IQNA)-Waislamu katika mji mkuu wa Iceland, Reykjavik wanafunga masaa 22 kwa siku katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na usiku kuwa mfupi katika ncha ya kaskazini duniani.

TEHRAN (IQNA)-Waislamu katika mji mkuu wa Iceland, Reykjavik wanafunga masaa 22 kwa siku katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na usiku kuwa mfupi katika ncha ya kaskazini duniani.

Iceland ni nchi iliyo katika kisiwa kaskazini mwa Bahari ya Atlantiki na ina wakaazi Waislamu wapatao 1,500 ambao huanza saumu ya Ramadhani saa nane usiku (wa manane) kwa majira ya Reykjavik na kuendelea kufunga hadi saa sita usiku na hivyo kutumiza masaa 22 ya saumu.

"Ingawa muda wa saumu hapa ni mrefu, lakini Waislamu hawahisi hilo kwa sababu hukutana pamoja katika Mwezi wa Ramadhani,” anasema Abdul-Aziz Ulvani, Imamu wa Kituo cha Kiislamu cha Iceland.

"Sisis ni kama familia. Wote huja hapa mapema. Sisi husoma Qur’ani na baada ya Iftar sote huswali Tarawih pamoja. Siku za kwanza tatu huwa ngumu lakini baada ya hapo hali huwa ya kawaida.”

Ncha ya kaskazini ya kijiografia iko katikati ya Bahari ya Aktiki. Ni mahali ambako mhimili wa kuzunguka kwa dunia unagusa uso wa dunia. Mahali hapa papo kwa anwani ya kijiografia ya 90°S na 0°W.

Usiku na mchana ina muda wa nusu mwaka. Macheo ya pekee hutokea kila mwaka tarehe 21 Machi na mchana unaendelea hadi 23 Septemba siku ya machweo. Jua halizami kabisa katika muda huo. Kinachofuata ni machweo na mwanga wa utusiutusi wa wiki kadhaa hadi giza imeanza kabisa inayoendelea hadi Machi.

http://iqna.ir/en/news/3463086

captcha