IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani yamalizika Tehran

14:08 - June 17, 2017
Habari ID: 3471021
TEHRAN (IQNA) –Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yamemalizika Ijumaa usiku katika sherehe iliyofanyika mjini Tehran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe hizo zilihudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran Bw. Sayyed Ridha Salehi Amiri pamoja na maafisa wa ngazi za juu ya kiutamaduni, kidini na harakati za Qur'ani.

Sherehe hizo zilizofanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Sala wa Imam Khomeini SA, zilianza kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu na kasha mkuu wa maonyesho hayo, Hujjatul Islam Muhammad Ridha Hishmati akawasilisha ripoti ya maonyesho hayo ya kimataifa ya Qur'ani.

Aliashiria maonyesho ya mwaka huu ni kusema mashirika sabu ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yalitoa ushirikiano katika kuandaa maonyesho hayo.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri w Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu alitangaza azma ya wizara yake kuendeleza utamaduni na mafundisho ya Qur'ani nchini Iran. Katika maonyesho hayo, Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) lilitangazwa kuwa shirika bora zaidi kwa mtazamo wa kuakisi habari za maonyesho hayo.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran ni makubwa ya aina yake duniani na huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran.

Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yalianza tarehe tatu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini SA mjini Tehran

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani yamalizika Tehran.

Maonyesho hayo ya kimataifa yamehudhuriwa na taasisi 50 na pia kuna mashirika zaidi ya 297 ya uchapishaji ambapo kati ya mashirika hayo, 281 ni kutoka Iran na 16 ni ya kimataifa kutoka nchi kama vile Uturuki, Iraq, Lebanon na Syria. Nchi zingine zilizoshiriki ni pamoja na Tunisia, Poland, Algeria, Kenya, Afghanistan, Bangladesh, India, Iraq na Senegal.

Kaulimbiu ya maonyesho ya mwaka huu ilikuwa ni "Qur'ani, Maadili na Maisha" na kwamba kutakuwa na hafla kadhaa kuhusiana na mada hii. Aidha mwaka huu kutakuwa na maonyesho maalumu yenye anuani ya: "Robo Karne ya Harakati za Qur'ani" ambapo washiriki watabainishiwa mafanikio ya maonyesho hayo ya kimataifa ya Qur'ani katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.

3610240

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani yamalizika Tehran
captcha