IQNA

Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Tanzania na Kenya+PICHA

11:04 - June 24, 2017
Habari ID: 3471033
TEHRAN (IQNA) Waislamu na watetezi wa haki Tanzania na Kenya wameungana na wapigania haki duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Maadhimisho hayo yamefanyika kuoneysha mshikamano wao na mapambano ya wananchi wa Palestina mbele ya maghasibu Wazayuni.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maandamano hayo jijini Dar es Salaam, Sheikh Hemedi Jalala Mkuu wa Chuo cha Kidini cha Imam Swadiq (as) cha Dar es Salaam Tanzania ameyataja maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwamba, yana umuhimu katika kufikisha ujumbe wa amani na kupinga dhulma za utawala vamizi wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

Sheikh Jalala mmoja wa wanaharakati wa Kiislamu nchini Tanzania amesema kuwa, Imam Khomeini (MA) muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani iwe ni siku ya kukumbuka vitu viwili. Kitu cha kwanza ni kuukumbuka msikiti mtakatifu wa al-Aqsa kibla cha kwanza cha Waislamu. Sheikh Hemedi Jalala ameongeza kuwa, jambo la pili ni kwamba, Imam Khomeini alitaka siku hii iwe ni maalumu kwa ajili ya kuwakumbuka wanyonge wote na watu wote wanaodhulumiwa duniani wakiwemo wananchi wa Palestina.

Huko Zanzibar pia Siku ya Quds imefanyika na kuhutubiwa na mwanahistoria na mwandishi maarufu wa Tanzania Bw. Mohammad Said. Katika hotuba yake, aliashiria historia ya kukaliwa kwa mabavu Palestina na msimamo wa kupinga Uzayuni wa mwanzilishi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Aidha Bw. Mohammad Said amesema ukombozi wa Palestina ni tamanio la kila mwislamu.

Mwambata wa utamaduni katika ubalozi wa Iran nchini Tanzania Bw. Ali Baqeri amehutubu katika mkutano huo wa Siku ya Quds mjini Zanzibar na kusema, "Siku ya Kimataifa ya Quds inatikisa misingi ya utawala wa Kizyauni wa Israel. Amesema tangu ilipokaliwa kwa mabavu Palestina na Quds Tukufu, kuliibuka mwamko na mapambano ya watu wa Palestina, Waislamu na wapenda uhuru kote duniani."

Katika mji mkuu wa Kenya, Waislamu na wasiokuwa Waislamu wamekusanyika katika ukumbu wa Sir Ali Muslim Club katika Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo imeandiliwa na Kamati ya Siku ya Quds Kenya ainayojumuisha Jumuiya ya Waislamu ya Mahdi, Harakati ya Mshikamano na Palestina Kenya na Jumuiya ya Amani Afrika. Katika mji wa Mombasa nchini Kenya Waislamu pia wameshiriki katika Siku ya Kimataifa ya Quds ambapo wamesisitiza kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel. Pia wameikabidhi serikali ya Kenya taarifa ya kutaka nchi hiyo iunge mkono harakati za ukombozi Palestina.

Waislamu wa Nigeria, Tunisia, Afrika Kusini, Zimbabwe na maeneo mengine pia wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds.

Siku ya Kimataifa ya Quds  nchini Tanzania na Kenya+PICHA

Wanawake katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, Dar es Salaam

Siku ya Kimataifa ya Quds  nchini Tanzania na Kenya+PICHA

Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, Dar es Salaam


Siku ya Kimataifa ya Quds  nchini Tanzania na Kenya+PICHA

Siku ya Kimataifa ya Quds, Dar es Salaam


Siku ya Kimataifa ya Quds  nchini Tanzania na Kenya+PICHA

Siku ya Kimataifa ya Quds, Zanzibar, Tanzania


Siku ya Kimataifa ya Quds  nchini Tanzania na Kenya+PICHA

Siku ya Kimataifa ya Quds, Zanzibar, Tanzania


Siku ya Kimataifa ya Quds  nchini Tanzania na Kenya+PICHA

Siku ya Kimataifa ya Quds, Nairobi Kenya


3612432

3612363

captcha