IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Radio Bilal nchini Uganda

18:40 - June 28, 2017
Habari ID: 3471040
TEHRAN (IQNA)-Radio Bilal nchini Uganda imeandaa mashindano ya Qur'ani yaliyofanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa Iran mjini Kampala yalijumuisha wanafunzi 80 wasichana na wavulana kutoka maeneo mbali mbali ya Uganda ambao walishindana kwa muda wa siku 20.

Katika siku ya mwisho ya mashindano walioshika nafasi za kwanza hadi tatu walipata zawadi na kuenziwa katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Baraza Kuu la Waislamu Uganda.

Sherehe za kufunga mashindano hayo zilihudhuriwa na Mufti wa Uganda Sheikh Ramadhan Mubajje, Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa Iran mjini Kampala Ali Bakhtiari, Mkurugenzi wa Radio Bilal Mussa Mugerwa, Mkurugenzi wa Televisheni ya Kiislamu ya Salam TV ya Uganda Hajj Kareem Kalisa na wanazuoni wengine wa Kiislamu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mufti wa Uganda Sheikh Ramadhan Mubajje amebainisha furaha yake kutokana na kuimarika harakati za mashindano ya Qur'ani nchini nchini. Halikadhalika ameushukuru Ubalozi wa Iran mjini Kampala kwa kuunga mkono harakati za Qur'ani nchini humo.

3613754

captcha