IQNA

Kikao cha Siri cha nchi za Kiarabu na Utawala haramu wa Israel kuhusu Ukanda wa Ghaza

13:33 - June 29, 2017
Habari ID: 3471041
TEHRAN (IQNA)- Kumefanyika kikao cha siri mjini Cairo kati ya nchi kadhaa za Kiarabu na Utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu mustakabali wa eneo la Palestina la Ukanda wa Ghaza.

Duru zinadokeza kuwa, kikao hicho cha siri kimefanyika wiki iliyopita lakini hadi sasa maelezo kamili kuhusu mkutano huo hayajabainika.

Gazeti la Misri la Rai Al Youm limeandika kuwa, mazungumzo hayo yalikuwa ya kiusalama na yenye umuhimu mkubwa na kwamba yaliandaliwa na Shirika la Kijasusi la Misri. Imearifiwa kuwa mkutano huo ulihudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa mashirika ya kijasusi ya pande husika huku Marekani nayo ikituma muwakilishi katika kikao hicho. Nchi za Kiarabu zilizoshiriki katika mkutnao huo ni mwenyeji Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia na Jordan.

Misri na Jordan zina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel huku UAE zikiwa na uhusiano wa siri na utawala huo ghasibu. Nchi hizo za Kiarabu zimekuwa zikichukua maamuzi yaliyo kinyume cha maslahi ya Wapalestina kwa lengo la kuwaridhisha Wamarekani na Wazayuni na kwa msingi huo kikao hicho cha faragha kuhusu Ghaza bila shaka ni kwa madhara ya wakaazi wa eneo hilo ambalo liko chini ya mzingiro wa Israel tokea mwaka 2007.

3613839

captcha