IQNA

Watu 158 Wasilimu nchini Oman

22:38 - July 07, 2017
Habari ID: 3471055
TEHRAN (IQNA)-Watu 158 wamesilimu nchini Oman katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Kwa mujibu wa Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini nchini Oman, watu 158 walikumbatia dini tukufu ya Kiislamu maishani nchini humo katika miezi ya Aprili, Mei, Juni.

Taarifa zinasema waliosilimu ni raia wa Uganda, Ufilipino, Sri Lanka na India huku aghalabu wakiwa ni wanawake.

Baadhi walisilimu hivi karibuni katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati wa hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya waliosilimu. Idadi kubwa ya waliosilimu wanasema Uislamu umetoa jibu muafaka kwa matatizo yao maishani huku wakishukuru namna Waomani walivyowakumbatia. Kwa mfano, Jubelyn Alto ambaye ni raia wa Ufilipino anasema aliufahamu Uislamu katika kipindi cha miezi miwili tu na akaamua kusilimu.

"Nilikuja Omba miaka miwili na nusu iliyopita na miezi miwili iliyopita nukaamua kusoma Uislamu kwani nilihisi kuwa na mzigo mkubwa wa matatizo.” Anasema baada ya kusilimu alipata utulivu mkubwa na kutokana na muongozo wa Qur’ani Tukufu.

Katika halfa ya kuutangaza Uislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jumla ya watu 15 walisilimu nchini Oman.

3463285

captcha