IQNA

Waislamu 6,000 Wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Dunia Kimya

14:11 - August 04, 2017
Habari ID: 3471103
TEHRAN (IQNA)-Zaidi ya Waislamu 6,000 wameuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati tokea mwaka 2013 lakini jamii ya kimataifa imenyamazia kimya jinai hiyo na kuonyesha kutojali.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetaja hatua ya Wakristo wenye misimamo mikali wa kundi la Anti-Balaka kuwaua Waislamu kuwa ni ‘mauaji ya kimbari’.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) yaliibuka mwaka 2013, baada ya waasi wa Seleka kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo,François Bozizé. Baada ya rais Mwislamu, Michel Djotodia kuchukua mamlaka, waasi wa Kikristo wenye kufurutu ada wa Anti-Balaka walianzisha mauaji ya kutisha dhidi ya jamii ya Waislamu, ambapo maelfu ya watu waliuawa na wengine wengi kuwa wakimbizi.Djotidia alilazimishwa na nchi za kieneo kujiuzulu Janarui mwaka 2014 na hapo mauaji ya Waislamu yakashika kasi zaidi. Kabla ya kuanza mgogoro, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, ulikuwa na wakaazi 130,000 Waislamu lakini sasa taarifa zinasema idadi hiyo ni chini ya 1,000.

Aidha watu zaidi ya 400,000, wengi wakiwa ni Waislamu wamelazimika kukimbia makazi yao huki wengine milioni 2.7, au nusu ya watu wote CAR wanahitaji msaada. Mauaji ya Waislamu CAR yanajiri pamoja na kuwepo vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini humo.

3626373/

captcha