IQNA

Wahudumu wa Haram Tukufu ya Imam Ridha AS wakutana na Ulamaa wa Ahlul Sunna Zanzibar

0:44 - August 05, 2017
Habari ID: 3471104
TEHRAN (IQNA) Kwa munasaba wa Wiladat ya Imam Ridha AS, Msafara wa wahudumu wa Haram Takatifu ya Imam Ridha AS iliyoko mjini Mashhad nchini Iran wamefika Zanzibar nchini Tanzania na kukutana na Ulamaa wa Ahul Sunna.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe za kukumbuka kuzaliwa Imam Ridha AS, mjukuu wa Mtume Muhammad SAW na Imam nane katika Madhehebu ya Ahul Bayt AS zimefanyika katika Kituo cha Elimu cha Ahul Bayt AS kinachosimamiwa na Taasisi ya Bilal Muslim Mission huko Zanzinbar.

Katika sherehe hiyo awali aya za Qur’ani Tukufu zilisomwa na qarii kutoka Iran aliye katika msafara huo na baada ya hapo Sheikh Ishaq katika kituo hicho cha elimu alitoa mawaidha kuhusu maisha ya Imam Ridha AS.Wahudumu wa Haram Tukufu ya Imam Ridha AS wakutana na Ulamaa wa Ahlul Sunna Zanzibar

Wengine waliozungumza katika hafla hiyo ni Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bw. Ali Bagheri na Hujjatul Islam wal Muslimin Khusropanah ambapo walibainisha kuhusu fadhila za Imam Ridha AS na udharura wa itikadi ya Uimamu. Katika hafla hiyo pia kulizinduliwa bendera ya Haram Takatifu ya Imam Ridha AS ambapo hadhirina walipata fursa ya kutabaruku.

Halikadhalika msafara huo kutoka Haram Tukufu ya Imam Ridha AS pia ulikutana na Sheikh Fadhil Sulaiman Katibu wa Mufti wa Zanzibar na kubadilishana mawazo kuhusua masuala ya umoja wa Waislamu.Wahudumu wa Haram Tukufu ya Imam Ridha AS wakutana na Ulamaa wa Ahlul Sunna Zanzibar

Katika mkutano huo, Ali Bagheri aliashiria kuchaguliwa mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran kuwa mji mkuu wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu barani Asia mwaka 2017 na kusema: "Mashhad ni mji wa elimu na alipolazwa Mjukuu wa Mtume SAW na hivyo msafara unaotembelea Tanzania unabeba ujumbe wa umoja na udugu kutoka mji mkuu wa kiutamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu.”

Kwa upande wake Hujjatul Islam Khosropanah aliye katika msafara huo alisema: "Sisi tumebeba ujumbe wa umoja na udugu kutoka ardhi takatifu alikolazwa Mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Aliongeza kuwa Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisisitiza sana kuhusu umoja wa Waislamu duniani na hivyo Iran inatoa wito kwa wafuasi wa dini zote kudumisha amani na umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu.

Kwa upande wake naibu Mufti wa Zanzibar ameashiria kuwepo umoja baina ya wafuasi wa madhehebu na dini mbali mbali Zanzibar. Ameongeza kuwa kuna baraza la kidini Zanzibar ambalo lina jukumu la kuhakikisha kunadumishwa maelewano baina ya wafuasi wa dini na madhehebu zote.Wahudumu wa Haram Tukufu ya Imam Ridha AS wakutana na Ulamaa wa Ahlul Sunna Zanzibar

Itakumbukwa kuwa, tarehe 11 Dhulqaad mwaka 148 Hijria Qamaria, miaka 1290iliyopita, alizaliwa Imam Ali bin Mussa Ridha AS, mmoja kati ya Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad katika mji wa Madina. Imam Ridha alichukua jukumu la kuwaongoza Waislamu mara baada ya kufariki dunia baba yake, Imam Mussa al-Kadhim AS mnamo mwaka 183 Hijiria. Shakhsia huyo alikuwa mbora zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu wakati na zama zake. Historia inasema kuwa Imam Ridha kama walivyokuwa mababa na mababu zake watukufu AS alianisika mno na Qur’ani na hakuacha kusoma kitabu hicho popote pale alipokuwa.

Wahudumu wa Haram Tukufu ya Imam Ridha AS wakutana na Ulamaa wa Ahlul Sunna Zanzibar

3626468

captcha