IQNA

Tajikistan yapiga Marufuku Hijabu katika kampeni dhidi ya Uislamu

23:03 - August 07, 2017
Habari ID: 3471110
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Tajikistan imetangaza kuwazuia wanawake wa nchi hiyo kuvaa vazi la staha la Hijabu ikiwa ni muendelezo wa vita dhidi ya Uislamu.
Kufuatia amri hiyo, vitengo maalumu vya kukabiliana na vazi la hijabu katika mji mkuu wa nchi hiyo, Dushanbe vimekuwa vikito vitisho na kuwatoza faini kubwa ya fedha wanawake wanaovaa vazi hilo.

Aidha polisi wa miji tofauti ya Tajikistan wanaendesha operesheni ya kutaka kuwavua vazi hilo wanawake wanaojisitiri.

Ni suala lisilo na shaka kwamba, kuendelea mwenendo huu, kuna maana ya kufuatwa siasa zisizo sahihi nchini humo. Athari za ufuataji siasa hizo potofu zinaweza kuonekana katika matamshi aliyotoa Rais Emomali Rahmon wa Tajikistan yapata miaka miwili iliyopita wakati alipokutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha mji wa Kulob nchini humo. Katika hotuba yake, Rais Rahmon alisema: "Mnadhania kwamba kwa kuvaa hijabu na kujistiri, ndio mtaenda peponi? au kwamba kwa kuvaa kwenu vazi la hijabu mtasamehewa madhambi yenu?"

Misikiti pia yasakamwa

Wakati huo huo baadhi ya misikiti imesimamishwa kuendesha shughuli zao za kidini nchini Tajikistan, nchi ambayo zaidi ya asilimia 98 ya watu wake ni Waislamu, kwa kisingizio cha kutokuwa na hati za kisheria.

Kampeni ya kupiga vita Uislamu nchini Tajikistan ilianza kwa lengo la kile kilichodaiwa na viongozi wa nchi hiyo kuwa ni kupambana na misimamo ya kufurutu mpaka.

Tajikistan ni nchi ndogo ya Asia ya Kati ambayo haina pwani kwenye bahari yoyote. Imepakana na Uchina, Afghanistan, Uzbekistan na Kyrgyzstan na idadi ya watu wake inakadiriwa kuwa milioni 8.6.

Mwaka 1868 Tajikistan ilivamiwa na Urusi na kuwa sehemu ya Dola la Urusi, halafu sehemu ya Umoja wa Kisovyet baada ya mapinduzi ya 1917. Iliitwa Jamhuri ya Kisovyet ya Kisoshalisti ya Tajikistan. Baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisoviet, Tajikistan ilipata uhuru wake mwaka 1991.

3626013

captcha