IQNA

Oman yasomesha Qur’ani Tukufu kupitia Intaneti

12:05 - August 08, 2017
Habari ID: 3471112
TEHRAN (IQNA)- Oman imepanga kuanzisha mafunzo ya kusoma Qur’ani Tukufu kupitia intaneti kwa Waislamu wote.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, usajili wa wanaotaka kushiriki katika kozi hiyo umeanza tarehe 5 Agosti na utaendelea hadi 30 Agosti.

Kwa mujibu wa Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini nchini Oman, mbinu mpya za kufunza Qur’ani kwa kutegemea teknolojia za kisasa zitatumika katika kozi hiyo na hivyo Waislamu hasa waliosilimu watapa fursa ya kujifunza misingi ya Qur’ani na pia kuhifadhi Kitabu hicho kitukufu.

Mpango wa kuandaa kozi hiyo ya Qur’ani kwa njia ya intaneti ulianza kuratibiwa miaka mitatu iliyopita na sasa umekamilika. Kati ya malengo mengine yaliyotajwa katika kuanzisha kozi hiyo ni kueneza utamaduni wa Kiislamu, kuwahimiza vijana na mabarobaro wahifadhi Qur’ani Tukufu na pia kuwawezesha kutafakari kuhusu mafundisho ya Qur’ani Tukufu. Kozi hiyo inatazamiwa kuanza Septemba 4.

3626818

captcha