IQNA

Mahuhaji Trinidad na Tobago wataka ukumbi wa kusalia uwanja wa ndege

12:22 - August 09, 2017
Habari ID: 3471113
TEHRAN (IQNA)-Waislamu nchini Trinidad na Tobago wametoa wito kwa wasimamizi kwa mamlaka ya viwanja wa ndege nchini humo ichukue hatua za dharura za kuwaandalia Mahujaji chumba maalumu cha kusali.

Wito huo umetolewa na Imtiaz Mohammed Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu nchini humo ijulikanayo kama Ummah T&T Muslim Lobby Group. Amesema kwa kuzingatia idadi kubwa ya watu wanaofika uwanja wa ndege kuwaaga mahujaji kuna haja ya wakuu wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege Piarco kuandaa ukumbi maalumu wa kusali kwa mahijaji na wanaokuja kuwaaga.

Amesema Waislamu wanadhalilishwa kwa kusali katika sehemu mbali mbali za uwanja wa ndege zinazotumiwa na wasafari jambo linalotzamwa kama bugudha na wasafiri wengine. Amesema Waislamu wana haki ya kikatiba ya kupata sehemu maalumu ya kuswali katika uwanja wa ndege.

Imtiaz Mohammed amesema kile mwenye kuhiji kutoka Trinidad na Tobago analipa takribani dola za kimarekeni 8,900 na hivyo wakuu wa uwanja wa ndege wanapaswa kuwaandalia mazingira tulivu katika uwanja wa ndege.

Hatahivyo mamlaka ya viwanja wa ndege nchini humo imepinga ombi hilo la Waislamu na kudai kuwa hakuna dini yoyote inayoruhusiwa kuwa na sehemu maalumu ya ibada.

Jamhuri ya Trinidad na Tobago ni nchi ya visiwani katika Karibi ya kusini, karibu na pwani ya Venezuela, kusini kwa kisiwa cha Grenada cha Antili Ndogo. Nchi jirani nyingine kuvukia bahari ni Barbados na Guyana.

Nchi ina eneo la km² 5,128 ambalo karibu lote ni kisiwa kikuu cha Trinidad. Kile cha Tobago kina asilimia 6 tu za eneo pamoja na 4% ya wakazi. Kuna visiwa vidogo vingine 21.

Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia tano ya watu wote 1.3 million nchini Trinidad and Tobago.

3463600
captcha