IQNA

Kozi ya walimu wa Qur'ani nchini Senegal

17:36 - August 09, 2017
Habari ID: 3471114
TEHRAN (IQNA)-Kozi ya kiwango cha juu ya walimu wa Qur'ani nchini Senegal imefanyika katika mji wa Touba kati mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kozi hiyo imeandaliwa na kituo cha utamaduni cha Iran nchini Senegal kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kitaifa ya Shule za Qur’ani Senegal pamoja na Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu Iran, (ICRO).

Kozi hiyo iliongozwa nana mtaalamu maarufu wa Tajwidi kutoka Iran Ustadh Majid Zakilou ambapo waalimi 30 wa Qur'ani Tukufu kutoka mikoa mitatu ya Senegal walishiriki katika mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika Agosti 2-4.

Washiriki walipata chetu cha ushiriki na zawadi ya nakala ya Qur'ani Tukufu iliyochapishwa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mji wa Touba una idadi ya watu zaidi ya 550,000 na ni wa pili kwa ukubwa Senegal baada ya mji mkuu Dakar.

Senegal ni nchi ya Kiislamu iliyo Afrika Magharibi na inapakana na Mauritania upande wa kaskazini, Mali upande wa mashariki, Guinea upande wa kusini mashariki, Guinea-Bissau upande wa kusini amgharibi huku ikiizunguka Senegal kwa pande tatu isipokuwa katika pwani.

3628235

captcha