IQNA

Watu milioni mbili watembelea Jumba la Makumbusho la Qur’ani Madina

14:08 - August 11, 2017
Habari ID: 3471118
TEHRAN (IQNA)-Mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la Qur’ani Tukufu katika mji wa Madina nchini Saudi Arabia limetembelewa na wageni milioni mbili katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa Hamza Musa Adam Mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la Qur’ani Tukufu, katika jumba hilo lina nakala nyingi zilizoandikwa kwa mkono na pia nakala 57 nadra za Qur’ani Tukufu.

Amesema nakala ya kale zaidi hapi ni iliyo iliyoandikwa mwaka 488 Hijria Qamaria (1095 Miladia). Aidha ameongeza kuwa moja ya nadra za Qur’ani katika maonyesho hayo ni ilie yenye uzito wa kilo 154 iliyoandikwa karne mbili zilizopita.

Adam amesema wageni katika Jumba la Makumbusho la Qur’ani Tukufu mjini Madina wanapokea maelezo kwa lugha 13. Amesema tokea kuanzishwa kwake mwaka 2015, jumba hilo la makumbusho limepokea wageni milioni mbili kutoka maeneo mbali mbali duniani huku idadi ya wanaofika hapo ikitazamiwa kuongezeka katika msimu wa Hija mwaka huu.

3628862/

captcha