IQNA

UN hatimyae yavunja kimya chake kuhusu kukandamizwa Mashia Saudia

23:03 - August 13, 2017
Habari ID: 3471119
TEHRAN (IQNA)- Hatimaye Umoja wa Mataifa umeutaka utawala wa Saudi Arabia usitishe jinai na hujuma zake dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia mashariki mwa nchi hiyo.

Stephane Dujarric, Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres, amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa, licha ya kuwa chombo hicho hakiwezi kuthibitisha ripoti za vyombo vya habari kuhusu jinai za Saudia huko al-Awamiya, lakini kingependa kuiona Riyadh inachukua hatua zisizokiuka haki za binadamu.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Waislamu hao wa madhehebu ya Shia waliutaka Umoja wa Mataifa uingilie kati ili kukomesha mashambulio ya maafisa usalama wa Riyadh dhidi yao. Wakaazi wa al- Awamiyyah walizitaka taasisi za kimataifa na za kisheria kuunda tume ya kutafuta ukweli ili kuchunguza vitendo vya ukandamizaji vinavyofanywa na utawala wa Aal Saud.

Tokea Mei 10 wanajeshi wa Saudi Arabia walivamia mtaa wa Al Mosara mjini Awamiyah katika wilaya ya Qatif mkoa mashariki mwa nchi hiyo ambapo tokea wakati huo wamewaua watu kadhaa na kuteteteza moto misikiti, nyumba za raia na shule katika mtaa huo. Aghalabu ya wakaazi wa eneo la Mashariki mwa Saudia ni Waislamu wa madhehebu ya Shia na wanakandamizwa na utawala wa ufalme wa Kiwahabbi wa Saudia.

Watawala wa Saudia wanadai wanataka kufanya ukarabati katika mtaa wa kihistoria wa al-Mosara ambako ndiko alikozaliwa Sheikh Nimri Baqir an-Nimr, mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu aliyeuawa kwa kukatwa kichwa na utawala huo mwaka jana.

Wataalamu wa masuala ya turathi katika Umoja wa Mataifa wameutaka utawala wa Saudia usitishe mpango wake wa kuubomoa mtaa huo wakisema ni wa kale na ni turathi ya utamaduni na ustaarabu wa eneo hilo. Hatahivyo watawala wenye kiburi wa Saudia wamepuuza kabisa agizo hilo la Umoja wa Mataifa na wanaendeleza na uharibifu wao.

3629054


captcha