TEHRAN (IQNA)-Msikiti wa Ahmad (Akhmad) Kadyrov uko mjini Grozny, ambao ni mji mkuu wa Jamhuri ya Chechenia nchini Russia.
Msikiti huo
ambao rasmi pia unajulikana kama "Roho ya Chechenia’ ni mkubwa zaidi nchini
Russia na umepewa jina la Akhmad Kadyrov, aliyeanzisha ujenzi wake akiwa meya
wa eneo la Konya.
Msikiti huo
una minara yenye urefu wa mita 62 na ujenzi wake unashabihiana na wa Msikiti wa
Sultan Ahmed wa mjini Istanbul, Uturuki,
Msikiti huo
ulifunguliwa rasmi mwaka 2008 katika sherehe iliyohutubiwa na kiongozi wa
Chechenia, Ramzan Kadyrov na kuhudhuria na waziri mkuu wa Russia wakati huo,
Vladimir Putin.