IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Marekani na Israel zinakiri uwezo wa Hizbullah umeimarika

23:23 - August 14, 2017
Habari ID: 3471122
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amesema kuwa, kushindwa na kufedheheka vitaukumba utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika vita yoyote ile itakayotokea, zaidi ya kushindwa kulikoukuta katika vita vya siku 33 vya mwaka 2006.
Sayyid Hassan Nasrallah aliyasema hayo jioni ya Jumapili ya jana mjini Beirut katika sherehe za mwaka wa 11 wa ushindi wa harakati ya harakati ya Hizbullah katika vita vya siku 33 mwaka 2006 kati ya harakati hiyo na utawala huo wa ghasibu wa Kizayuni na kuongeza kuwa, siku kama ya jana ni siku kubwa ambayo ndani yake wanamapambano wa Hizbullah walisimama imara na kufelisha njama na juhudi za askari wa Israel za kutaka kuikalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon amefafanua kuwa, muqawama hauna haja ya kufikia stratijia za kisiasa bali unafuatilia malengo makuu ya kitaifa na kwamba upande wowote unaovizia kutaka kuona muqawama huo unashindwa, basi utashuhudia hasara wenyewe, kama ambavyo pia upande wowote unaodhania kuwa mapambano (muqawama) ni dhaifu, basi utaishia kushindwa. Sayyid Hassan Nasrallah amesisitiza kuwa, wanamapambano shupavu wa muqawama katika vita ya siku 33 mwaka 2006 hawakuingia vitani kwa kutaka kujionyesha, bali kwa mapambano halisi ambayo hata baada ya kupita miaka 11 tangu kujiri vita hiyo, adui bado ameendea kuhisi fedheha na kukabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa muqawama huo. Kiongozi huyo wa Harakati ya Hizbullah amebainisha kwamba ugaidi, yaani Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unachora ramani juu ya maji ambayo itaishia kufeli. Sambamba na kuashiria kuwa Marekani na Israel zinasema kuwa Hizbullah ina uwezo mkubwa na hatarishi kwao,  amesema kama ninavyomnukuu: "Ndio ni kweli ina uwezo mkubwa, hususan juu ya njama za Israel."

Aidha Sayyid Hassan Nasrallah ameongeza kuwa, magaidi katika eneo wameletwa na Wamagharibi kwa kushirikiana na washirika wao na hata Rais Donald Trump katika kampeni zake za uchaguzi uliopita alikuwa akisisitizia sana suala hilo na ameongeza kwa kusema, Marekani ndio inayaunga mkono kifedha makundi ya kigaidi nchini Iraq na Syria na kwamba, hata hivyo njama hizo hazitaweza kuidhoofisha harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

3463636
captcha