IQNA

Warsha ya “Uislamu na Ukristo” yafanyika Zimbabwe

7:40 - August 16, 2017
Habari ID: 3471124
TEHRAN (IQNA)-Kituo cha utamaduni cha Iran nchini Zimbabwe kimeandaa warsha ya “Uislamu na Ukristo” mjini Harare.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, warsha hiyo imehudhuriwa na zaidi ya wanafunzi 50 wa vyuo vikuu Waislamu na Wakrsito. Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Harare amesema warsha hiyo imefanyika kwa ushirikiano na wasomi wa vyuo vikuu na makasisi Wakristo.

Sherehe za kufunga warsha hiyo zilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Elimu Zimbabwe, Mwambata wa Utamaduni wa Iran, mtaalamu wa kitengo cha kuutangaza Uislamu katika Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu Iran (ICRO) Hujjatul Islam Ali Mahdawi n a pia mtaalamu wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kiislamu katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran Hujjatul Islam Mukhtarian.

Akizungumza katika sherehe za kufunga warsha hiyo Naibu Waziri wa Elimu Zimbabwe amesema kuna haja ya warsha kama hizo nchini humo ili kuzuia kuenea makundi ya watu wenye misimamo mikali.

Waziri huyo alikabidhiwa zawadi ya kitabu chenye anuani ya "Mazungumzo ya Dini Zimbabwe” amebacho kimeandikwa na Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Harare. Aidha wanachuo walioshiriki katika warsha hiyo walipata vyeti vya ushiriki.

3629859


پایان دوره آموزشی «اسلام و مسیحیت» در زیمبابوه + عکس

captcha