IQNA

Wafungwa 21,000 wamehifadhi Qur’ani nchini Iran

23:42 - August 16, 2017
Habari ID: 3471126
TEHRAN (IQNA)-Wafungwa 21,000 wanaoshikiliwa katika magereza ya Iran wamehifadhi Qur’ani Tukufu.

Hayo yamedokezwa na Sheikh Ridha Rostani, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Utamaduni na Elimu katika Magereza ya Iran ambaye ameongeza kuwa, wafungwa hao kwa uchache wamehifadhi Juzuu tatu za Qur’ani Tukufu.

Akizungumza na mwandishi wa IQNA pembizoni mwa mashindano ya wafungwa mjini Khorramabad mkoani Lorestan magharibi mwa Iran, Sheikh Rostami amesema kuna mikakati kadhaa ya kuwafunza wafungwa Qur’ani Tukufu. Aidha amesema idara anayosimamia imeanzisha vituo 294 ya kufunza Qur’ani vijulikanavyo kama Dar ul Qur’an katika magereza kote Iran huku akisisitiza kuhusu ulazima wa kuongeza vituo hivyo ili kubadilisha maisha ya wafungwa.

Tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979, harakati za Qur'ani zimeimarika kote Iran huku idadi ya waliohifadhi Qur'ani ikizidi kuongezeka kila mwaka katika sekta zote za mfumo wa Kiislamu. Hivi sasa Iran iko mstari wa mbele katika ulimwengu wa Kiislamu katika kuhimiza uenezwaji utamaduni wa Qur'ani Tukufu.

3631001

captcha