IQNA

Kongamano la Kimataifa la Qur’ani na Hadithi kufanyika Indonesia

0:13 - August 17, 2017
Habari ID: 3471127
TEHRAN (IQNA)-Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Syarif Hidayatullah mjini Jakarta, Indonesia kimepanga kuandaa kongamano la kimataifa la Qur’ani na Hadithi baadaye mwaka huu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo litafanyika Novemba 6-8 na mada kuu itakuwa ni, "Hali ya Ustawi wa Masomo ya Qur’ani na Hadithi.” Aidha maudhui zingine zitakazojadiliwa katika kongamano hilo ni kama vile ‘Mbinu za masomo ya Qur’ani na Hadithi’, ‘Kuishi kwa msingi wa Qur’ani na Hadithi’, ‘Vyuo vya masomo ya Qur’ani na Hadithi’, ‘Qur’ani, Hadithi na Jinsia, Sayansi, Siasa, Vyombo vya Habari na Utamaduni’, pamoja na ‘Masomo ya Hadithi na Sayansi Indonesia.’

Kongamano hilo linalenga kuwaleta pamoja wasomi na watafiti wa taaluma mbali mbali katika uga wa Qur’ani na Hadithi. Halikadhalika pembizoni mwa kongamano hilo la kimataifa pia kutakuwa na mkutano wa pili wa kila mwaka wa Jumuiya ya Masomo ya Qur’ani Indonesia.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo unaweza kutembelea tovuti ya http://iconquhas.event.uinjkt.ac.id

3463661

captcha