IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Utatuzi wa kimantiki wa kadhia ya Palestina ni kura ya maoni

16:11 - June 11, 2018
Habari ID: 3471553
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hatima ya Palestina inapaswa kuamuliwa na Wapalestina wenyewe kupitia kura ya maoni yenye kuwajumuisha Wapalestina Waislamu, Wakristo na Mayahudi ambao wana asili na waliishi katika ardhi ya jadi ya Palestina.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei aliyasema hayo jana Jumapili, alipokutana na kundi la wahadhiri na wasomi hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa: "Daima tumekuwa tukisema kuwa, ili kuainisha serikali katika nchi ya kihistoria ya Palestina kunapaswa kutumiwa mbinu ambayo walimwengu wote wanaiafiki  yaani kufanyike kura na uchunguzi wa maoni  yenye kuwahusisha Wapalestina wote halisi ambao wako ndani au nje nchi ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu wawe ni Waislamu, Mayahudi au Wakristo ambao kwa uchache miaka 80 iliyopita walikuwa katika ardhi hizo"

Ayatullah Khamenei ameashiria ukweli huo na kuongeza kuwa: " Je, pendekezo hilo la Jamhuri ya Kiislamu, ambalo  limesajiliwa rasmi katika Umoja wa Mataifa linaendana na vigezo vya kimantiki vinayokubaliwa duniani au la? basi kwa nini nchi za Ulaya haziko tayari kufahamu hilo?

Kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni katika ukanda wa Ghaza,  Ayatullah Khamenei ameashiria safari ya hivi karibuni ya barani Ulaya ya waziri mkuu  wa utawala wa Kizayuni (Netanyahu)  na kumtaja muuaji watoto na Shimr wa zama hizi ambaye anajionyesha kuwa amedhulumuwa na kuongeza kuwa: "Mtenda jinai huyo ambaye ni kinara wa dhulma zote katika historia amewahadaa wakuu wa Ulaya kuwa eti Iran inataka kuwaangamiza Mayahudi milioni kadhaa katika hali ambayo pendekezo letu la utatuzi wa kadhia ya Palestina ni la kimantiki kabisa na ni mantiki inayoenda sambamba na demokrasia."

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu ameashiria sera na mwenedo wa undumakuwili wa madola makubwa yanayotumia mabavu ambayo yanaunga mkono tawala vamizi ambazo zimepelekea kulazimishwa vita na kuenea ugaidi na ukaliwaji mabavu sambamba na kuenea ukosefu wa amani katika eneo na dunia.

Akibainisha  kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi ya juu mionogni mwa wananchi wa mataifa mengi alisema: "Iran ya Kiislamu ina maadui zaidi miongoni mwa madola ya kiistikbari kama ambavyo ina ushawishi na uungaji mkono mkubwa miongoni mwa wananchi katika mataifa ya eneo. Jambo hilo limepelekea  maadui khabithi na wa daima watekeleze njama dhidi ya taifa la Iran na Jamhuri ya Kiislamu lakini kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu wataendelea kufeli."

3721744

captcha