IQNA

Kanisa Humburg Ujerumani Lageuzwa kuwa Msikiti

10:05 - September 28, 2018
Habari ID: 3471694
TEHRAN (IQNA)- Jengo moja ambalo limekuwa likitumiwa kama kanisa kwa muda mrefu mjini Humburg nchini Ujerumani sasa limegeuzwa na kuwa msikiti.

Katika sherehe iliyofanyika Jumatano, jengo hilo la kanisa sasa lilizinduliwa rasmi kama Msikiti wa An Noor na Waislamu sasa wameanza kutekeelza ibada hapo.
Mradi wa Msikiti wa An Noor ulianza mwaka 2013 na umekumbwa na utata. Jengo hilo lilikuwa likitumiwa na Wakristo kama Kanisa la Capernaum na kutokana na matatizo ya kifedha wasimamizi wake wakaamua kuliuzia kwa Kituo cha Kiislamu cha An-Noor.
Hatahivyo baadhi ya wakaazi wa mtaa wa Horn uliko msikiti huo mpya walipinga hatua ya Waislamu kununua jengo hilo ambalo limekuwa likihudumu kama kanisa tokea mwaka 1961.

Pamoja na hayo, aghalabu ya wakaazi wa mtaa huo wameunga mkono haki ya Waislamu kuwa na kituo chao cha ibada.
Idadi ya Wakristo wanaofungamana na mafundisho ya dini yao inazidi kupungua Ujerumani na maeneo mengine ya Ulaya huki idadi ya Waislamu ikiongezeka kwa kasi kubwa.

3749859

captcha