IQNA

Rais Macron wa Ufaransa atakiwa kuwasilikza Waislamu kuhusu sheria mpya

12:46 - October 01, 2018
Habari ID: 3471698
TEHRAN (IQNA)-Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametakuwa kusikiliza sauti za Waislamu kabla ya kukamilisha rasimu ya sheria mpya za Uislamu nchini humo.

Marwan Muhammad, mkuu wa zamani wa Muungano wa Kukabiliana na Chuki Dhidi ya Uislamu Ufaransa amesema serikali ya Ufaransa inapaswa kuamua iwapo utawatazama Waisalmu milioni 5 nchini humo kama wanaadamu wenye uwezo wa kujitegemea na kujiendeshea mambo yao.
Serikali ya Ufaransa kwa muda mrefu imekuwa ikitafakari kuhusu njia za kukabiliana na misimamo mikali ya kidini miongoni mwa Waislamu hasa wanaoishi katika mitaa duni yenye idadi kubwa ya wahajiri.
Mwezi Julai Rais Macron said ana mpango wa sheria ya kuhakikisha kuwa Uislamu utafuatwa maeneo yote nchini humo kw akuzingatia 'sheria za jamhuri'.
Serikali za mitaa zimetakuwa kufanya ushauriano wa umma kuhusiano na suala hilo.
Weledi wa mambo wanasema kutokana na sheria kali za kutegenisha kanisa na dola nchini Ufaransa na pia kukosekana uongozi moja unaotambulika katika Uislamu, imekuwa vigumu kuwepo na taasisi moja ambayo inaweza kuwa marejeo ya masuala yote ya Kiislamu nchini humo.
Uchunguzi wa maoni uliofanyika unaoneysha aghalabu ya Waislamu hawataku serikali ya Ufaransa ijuhusishe katika kuratibu masuala ya Waislamu.
Hivi karibuni kumetangazwa mpango wa serikali ya Ufaransa kutoza kile kinachotajwa kuwa ni 'Kodi ya Halal' ambayo itatumika kubuni na kuendesha taasisi ambayo itasimamua masuala ya Waislamu nchini humo.
Pendekezo la kodi hilo limetolewa na Taasisi ya Motaigne ambayo pia imependekeza kuwa lugha ya Kiarabu inapaswa kuingiza katika mtaala wa kitaifa wa masomo badala ya kufungwa misikitini tu kama ilivyo hivi sasa.
Rais Macron wa Ufaransa amesema katika kipindi cha wiki chache zijazo atatangaza utaratibu mpya ambao utahakikisha kuwa 'Uislamu unafuatwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri'.

3465202

captcha