IQNA

Hizbullah ya Lebanon

Vita vya "Seif al-Quds" vimethibitisha kuwa, Israel ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui

21:28 - May 22, 2021
Habari ID: 3473936
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, vita vya "Seif al-Quds" vimeonyesha kuwa, utawala haramu wa Israel ni dhaifu kuliko hata nyumba ya buibui.

Taarifa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah iliyotolewa Ijumaa imetoa pongezi kwa ushindi wa makundi ya wanamapambano na wananchi wa Palestina baada ya utawala ghasibu wa Israel kukubali kusitisha vita  dhidi ya Ukanda wa Ghaza bila masharti.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya Hizbullah ya Lebanon imesisitiza kuwa, wakati wa kujiri vita vya "Seif al-Quds' adui Mzayuni ametwishwa mahesabu mapya na kwamba, ushindi huu wa Palestina utakuwa na taathira kubwa katika vita na mapigano mengine katika eneo hili.

Kadhalika taarifa hiyo imebainisha kwamba, katika vita hivyo, wanamuqawama wa Palestina wamethibitisha kwamba, utawala ghasibu wa Israel una udhaifu na mapungufuu mengi katika nyuga mbalimbali za kijeshi na kiusalama.

Wakati huo huo, wananchi wa maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina wamejitokeza mapema asubuhi ya leo kushangilia ushindi wa taifa hilo mbele ya adui Mzayuni baada ya kutangazwa usishaji vita.

Baada ya siku 12 za hujuma na mashambulio ya kijeshi ya utawala vamizi wa Kizayuni wa Israel hatimaye utawala huo umeafiki mpango wa kusitisha vita.

Baraza la mawaziri la utawala bandia wa Israel limekubaliana na mpango wa kusitisha vita na tayari usitishai vita huo ulianza kutekelezwa usiku wa manane kuamkia Ijumaa ya leo kwa majira ya Ggaza.

3481261

captcha