IQNA

Qur'ani Tukufu iliyofasiriwa kwa lugha ya Kichina

16:38 - May 09, 2022
Habari ID: 3475229
TEHRAN (IQNA)- Nakala ya Qur'ani Tukufu iliyofasiriwa kwa lugha ya Kichina inahifadhiwa katika Kituo cha Bait-ul-Qur'an nchini Bahrain.

Nakala 1000 tafsiri hiyo ya Kichina ya Qur'ani Tukufu zimechapishwa hivi karibuni na kusambazwa miongoni mwa Waislamu wa China.

Nakala asili ya tafsiri hiyo iko katika Jumba la Makumbusho la Taipei, mji mkuu wa Taiwan.

Tafsiri hii ya  Qur'ani Tukufu iliandikwa na Hajj Abdul Rahman Ji Tuan na ina maelezo kuhusu baadhi ya aya.

Inaaminika kuwa Uislamu uliingia China katika karne ya saba Miladia ambapo Waislamu ni karibu asilimia 10 ya watu wote wa China. Baadhi ya takwimu zainaonyesha kuwa kuna Waislamu miliono 150 nchini China.

4055510

Habari zinazohusiana
Kishikizo: china qurani tukufu
captcha