IQNA

Waislamu India

Wahindu wenye misimamo mikali sasa wadai Taj Mahal ni hakalu lao

23:20 - May 21, 2022
Habari ID: 3475276
TEHRAN (IQNA) - Magenge ya Wahindu wenye msimamo mkali vinalenga kubomoa misikiti kote nchini India na sasa wanalenga jengo la kihistoria la Waislamu maarufu kama Taj Mahal.

Miaka 30 baada ya magenge ya Wahindu wenye misimamo mikali kubomoa msikiti wa kihistoria wa Babri mjini Faizabad, na kusababisha wimbi la umwagaji damu baina ya Waislamu na Wahindu ambapo maelfu ya watu waliuawa, sasa tena magenge ya  Wahindu wenye msimamo mkali wanakodolea macho maeneo mengine ya Waislamu -- hata Taj Mahal, turathi ya maarufu Waislamu duniani.

Wakiwa wamepewa ujasiri na utawala wa Waziri Mkuu Narendra Modi mwenye misimamo ya utaifa wa Kihindu, na pia wakisaidiwa na mahakama na uchochezi katikana mitandao ya kijamii, magenge hayo yanaamini misikiti kadhaa India ilijengwa juu ya mahekalu ya Kihindu, ambayo wanadai ni dini ya "kweli" ya India.

Hivi sasa hatari kubwa zaidi inaukabili msikiti wa Gyanvapi uliojengwa karne kadhaa huko Varanasi, ambao ni mojawapo ya miji mikongwe zaidi ulimwenguni  na ulipo mto Ganges ambao ni mtakatifu kwa Wahindu.

Wiki iliyopita ripoti zilidai uchunguzi ulioidhinishwa na mahakama kuhusu msikiti huo uligundua kuwa shivalinga, ambayo ni nembo ya mmoja ya miungu ya  Kihindu, shiva, kwenye eneo hilo.

"Hii ina maana hiyo ni sehemu hekalu," waziri wa serikali Kaushal Kishore, mwanachama wa chama cha Modi cha Bharatiya Janata (BJP), aliambia vyombo vya habari vya ndani, akisema kwamba Wahindu wanapaswa kufanya ibada zao hapo.

Waislamu tayari wamepigwa marufuku kutawadha katika tanki la maji ambapo masalio hayo ya Kihindu yanadaiwa kuwa.

Hofu iliyopo sasa ni kwamba eneo hilo la ibada la Kiislamu litakumbwa na hatima sawa na ya Msikiti wa Babri.

Ubomoaji huo pia ulikuza itikadi potovu ya Hindutva  ambayo inasisitiza Uhindu ni itikadi bora zaidi. Tukio la kubomolewa Msikiti wa Babari kimsingi  liliandaa njia ya kuinuka kwa Modi madarakani mnamo 2014.

Misingi ya msingi ya vuguvugu hilo kwa muda mrefu imekuwa kwamba Uhindu ndiyo dini asili ya India, na kwamba kila kitu kingine ni kigeni.

Sasa baadhi ya Wahindu wenye itikadi kali wanalenga kubomoa  Taj Mahal, eneo ambalo ni turathi ya kimatiafa iliyo katika orodha ya UNESCO.

Taj Mahal ni moja ya maeneo maarufu zaidi  ya kitalii duniani  na huwavutia mamilioni ya wageni kila mwaka.

Taj Mahal  kimsingi ni  jengo lenya mvuto la kaburi lenye umbo la msikiti mjini Agra na ni kati ya majengo mazuri duniani.

Taj Mahal ilijengwa 1631 - 1648 kwa amri ya Shah Jahan aliyekuwa mtawala wa nasaba ya Moghul aliyetaka kumkumbuka mke wake mpendwa  Mumtaz Mahal. Shah Jahan aliwaajiri mafundi 20,000 kutoka Asia ya Kusini na Asia ya Kati wakiongozwa na Mwajemi Ali Fazal. Msanifu huyu aliunganisha sifa za ujenzi wa Uajemi na Uhindi.

Licha ya kuwa hakuna ushahidi wa kuaminika, Wahindu wenye misimamo mikali wadai kwamba  Taj Mahal ilikengwa  juu ya  hekalu la shiva.

Mwezi huu ombi la mahakama liliwasilishwa na mwanachama wa chama cha Modi akijaribu kulazimisha Shirika la Kiakiolojia la India, ASI, kufungua vyumba 20 ndani Taj Mahal, wakiamini kuwa vina sanamu za Kihindu.

ASI ilisema hakukuwa na sanamu kama hizo na mahakama ilitupilia mbali ombi hilo.

Hatahivyo inaonekana Wahindu wenye misimamo mikali wataendeleza njama zao dhidi ya Taj Mahal.

3478976

Habari zinazohusiana
Kishikizo: taj mahal india bjp wahindu
captcha