IQNA

Msomi wa Algeria

Umoja ni Lazima kwa Umma wa Kiislamu

20:06 - June 22, 2022
Habari ID: 3475409
TEHRAN (IQNA) – Msomi na mwanafikra wa Qur’ani wa Algeria anasema umoja baina ya nchi za Kiislamu ni jambo la lazima na unapaswa kufikiwa katika nyanja tofauti.

"Nguvu na uhuru wa Waislamu unategemea umoja wao na hivyo kutambua na kufikia umoja huu ni lazima," Nureddin Abu Lahya aliiambia Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA).

Ipo haja ya Waislamu kujumuika pamoja katika nyanja tofauti za utamaduni, siasa na uchumi, alisema na kuongeza kuwa umoja una vigezo tofauti vikiwemo umoja wa watu wengi ambao ni umoja baina ya mataifa ya Kiislamu, na umoja wa kifikra ambao una fikra moja,  umoja wa kiuchumi ambao unatumia uwezo wa pamoja wa kiuchumi kufikia malengo ya Umma wa Kiislamu, na umoja wa kisiasa ambao ni kuwa na utawala mmoja wa kisiasa au kuwepo kwa miungano ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa mwanazuoni huyo, Umma wa Kiislamu unakabiliwa na changamoto za ndani na nje katika njia ya kufikia umoja

Alitaza migongano au misugano ya kimadhehebu na kujisalimisha kwa maadui kuwa ni changamoto mbili za ndani huku akizitaja sera za madola ya kibeberu na ubaguzi katika nchi za Magharibi kuwa changamoto mbili za kigeni katika umma wa Kiislamu.

Katika sehemu nyingine amepongeza fatwa ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei inayoharamisha matusi yoyote kwa matukufu ya Waislamu wa Kisuni na kusema kuwa, hatua hiyo inalenga kuzuia fitna na migawanyiko.

Siku ya 17 ya Rabi al-Awwal, ambayo inaaminika na Waislamu wa Shia kuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (SAW), wakati Waislamu wa Sunni wanaichukulia siku ya 12 ya mwezi  huo kama siku ya kuzaliwa Mtume Huyo Mtukufu wa Uislamu.

Hayati Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini –Mwenyezi Mungu Amrehemu- alitangaza muda wa baina ya siku hizo mbili kuwa Wiki ya Umoja wa Kiislamu.

Tokea atoe tangazo hilo muongo wa thamani hufanyika mijimuiko na makongamano ya kuhimiza umoja na mshikamano wa Waislamu kote duniani.

4013249

captcha