IQNA

Sura za Qur'ani /9

At-Tawba, Sura pekee katika Qur'ani ambayo haijaanza kwa 'Bismillah'

10:55 - June 23, 2022
Habari ID: 3475414
TEHRAN (IQNA) – Sura zote ndani ya Qur’ani Tukufu zinaanza na sentensi “Kwa Jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu” (Bismillah Ar-Rahman Ar-Raheem) isipokuwa Sura At-Tawbah.

Pia inajulikana kama Bara'ah, hii ni sura ya 9 ya Qur'ani Tukufu na ina aya 129. Sura hiyo imeteremshwa Madina na iko katika Juzuu za 10 na 11 za Qur'ani. Kwa kadiri mfuatano wa wahyi unavyohusika, hii ni sura ya 114, yaani sura ya mwisho iliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

Tawbah kwa Kiarabu ina maana ya toba na katika istilahi ya Qur'ani inahusu kurudi kutoka kwa dhambi kuelekea kwa Mwenyezi Mungu. Aya nyingi za sura hii zinazungumza juu ya toba na hii ndio sababu ya jina lake. Miongoni mwa sifa muhimu zaidi za sura hii ni kwamba inaanza bila ya “Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu” na wafasiri au mufasirina na wanazuoni wametaja sababu mbalimbali za hili:

- Ibara ya"Kwa Jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu" inalenga kurehemu lakini surah inaonya juu ya matokeo ya kuepuka toba.

Toba ndilo lengo kuu la surah hii kwani inatoa muongozo wa Tawba halisi kwa kuzingatia matendo kama vile Sala, Zakat, na Jihadi.

Sura hiyo pia inagusia baadhi ya madhambi kama vile kupenda anasa za kidunia, uvivu, udanganyifu, na uwongo na haya ni mambo ambayo hayazingatiwi kuwa ni madhambi makubwa na kwa kawaida hutendwa na hata wale wanaodai kuwa Waislamu na kujifanya kuwa wanashikamana na maadili ya kidini. Katika Qur'ani Tukufu, madhambi hayo yamefananishwa na uasherati na ukafiri.

Sura hii inawaamrisha waumini kukata mafungamano na makafiri huku wakiweka wazi njia ya toba. Sura inawausia Waumini wajiepushe na makafiri walio karibu nao kama vile Nabii Ibrahim alikaa mbali na baba yake.

Hadithi ya Masjid al-Dirar ni miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika sura hii; Msikiti huo ulikuwa umejengwa na wanafiki ili kuzusha mifarakano baina ya Waislamu na baadaye ukavunjwa kwa amri ya Mtume Muhammad (SAW).

Habari zinazohusiana
captcha