IQNA

Haki za Binadamu

Shireen Abu Akleh na Mandla Mandela watunukiwa Tuzo ya Haki za Binadamu za Kiislamu

15:54 - August 03, 2022
Habari ID: 3475573
TEHRAN (IQNA)- Katibu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Idara ya Mahakama ya Iran amesema, tuzo ya saba ya mkutano wa kila mwaka wa Haki za Binadamu za Kiislamu atatunukiwa mwandishi wa habari Shahidi Shireen Abu Akleh na Mandla Mandela mpigavita ubaguzi wa rangi wa Apathaidi katika kuwaunga mkono watu wa Palestina.

Tuzo ya Haki za Binadamu za Kiislamu na Heshima ya Kiutu, ni tuzo ya heshima inayotolewa na Tume ya Haki za Binadamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa wanaharakati watetezi wa haki za binadamu au waathirika wa ukiukaji haki za binadamu, (wawe watu binafsi au shakhsia wenye nyadhifa), bila kujali dini, rangi, jinsia au utaifa wao.

Kwa mujibu wa taarifa, Kazem Gharib Aabadi, Katibu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Idara ya Mahakama ya Iran amesema kuhusiana na hafla ya mkutano wa kila mwaka wa haki za binadamu za Kiislamu kwamba: Tangazo la Haki za Binadamu za Kiislamu ni matokeo ya juhudi zilizofaywa na nchi za Kiislamu kwa lengo la kubuni mpango wa ulimwengu nzima wa haki za binadamu.

Mandla Mandela

3479971

 

captcha