IQNA

Sala ya mvua

Waislamu wa Ufaransa waombea mvua huku ukame usio wa kawaida ukikumba Ulaya

16:25 - August 15, 2022
Habari ID: 3475625
TEHRAN (IQNA) - Waislamu wa Ufaransa wameombea mvua wakati nchi hiyo, pamoja na mataifa mengine ya Ulaya, yakikumbwa na kile kilichotajwa kuwa ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 500.

Ukame wa kipekee unaathiri Ufaransa na majirani zake kwa karibu miezi miwili, bila mvua kubwa katika Magharibi, Kati na Kusini mwa Ulaya.

Rais wa Baraza la Ufaransa la Dini ya Kiislamu (CFCM) Rhône-Alpes, Benaissa Chana, alizindua wito kwa misikiti siku ya Ijumaa Agosti 12 "kutoa muda kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi Mungu mvua, ”

Wito huo unalingana na ule uliozinduliwa na Muungano wa Misikiti ya Ufaransa (UMF) mapema mwezi huu.

"Maji ni muhimu kwa uhai, ni muhimu  kwa sayari yetu, kwa wanadamu na viumbe vingine na viumbe," Chana alisema.

“Mungu anaweza kufanya kila jambo liwezekane. Kwa rehema zake, tunaweza kumuomba atujaalie tunachohitaji (mvua), kama alivyotufundisha Mtume wa Uislamu (SAW),” aliongeza.

Ukame unaoathiri Ulaya unatarajiwa kuendelea katika kile ambacho wataalamu wanasema unaweza kuwa ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 500.

Sala maalumu ya Waislamu kwa ajili ya mvua ni desturi inayojulikana sana kutoka kwa mila ya Mtume Muhammad (SAW).

Sala ya Istisqa yaani Sala ya Kuomba Mvua ni ibada maalumu Kiislamu ya kujibu ukame kwa kumuomba Mwenyezi Mungu mvua ya kufufua ardhi.

3480100

captcha